Emblem TRA Logo
Riba, Adhabu ya uchelewaji na Makosa

Riba, Adhabu ya uchelewaji na Makosa


Kushindwa kufuata mahitaji ya vipengere mbalimbali vya sheria kunapelekea utozaji wa riba,adhabu ya uchelewaji katika kukomboa kodi.
Sehemu hii inatoa maelezo kuhusu riba na adhabu ya uchelewaji na jinsi ya usimamizi wake.
 

 

Riba
1. Riba kwa ajili ya makadirio pungufu ya kodi #

Walipa Kodi wa awamu wa kodi ya mapato wanaojikadiria kwa mwaka wa mapato wanategemewa kuonyesha kiwango cha juu cha usahihi katika makadirio yao. Kushindwa kukadiria kodi katika muda unaostahili matokeo yake ni makadirio pungufu na kunapelekea utozwaji wa riba. Kiwango cha riba kinatozwa kwa kila mwezi.


2. Riba kwa ajili ya kushindwa kulipa Kodi
Ikiwa kiwango chochote kilichotozwa kodi chini ya sheria yoyote ya kodi kitakachokuwa hakijalipwa baada ya siku ya mwisho ya kulipa kodi kadri inavyohitajika kwa mujibu wa sheria za kodi au kanuni inapelekea utozwaji wa riba. Riba itatozwa kwa kiwango cha riba kwenye kiwango cha kodi kinachodaiwa katika kipindi husika. Kama wakala wa kodi ya zuio atashindwa kulipa koi ya zuio, hawezi kuikomboa kwa mtu aliyemkata kodi hiyo.
 

 

Adhabu ya uchelewaji


1. Kushindwa kutunza kumbukumbu
 

Kushindwa kutunza kumbukumbu zinazostahili kama zinavyohitajika kwa mujibu wa sheria kunapelekea utozaji wa adhabu ya uchelewajikwa kila mwezi au sehemu ya mwezi wakati kosa linaendelea kutendeka. Adhabu ya uchelewaji kwa mtu binafsi atatozwa pointi za sarafu 1 na kwa Kampuni itatozwa pointi za sarafu 10. Kiwango cha kodi kinachotakiwa kwa kipindi fulani na kwa namna kodi iliyokadiriwa inavyogawanywa.
 

2. Adhabu ya kushindwa kuwasilisha Ritani
 

Kushindwa kuwasilisha ritani au kulipa kodi wakati wa siku ya mwisho ya kulipa kodi kunapelekea utozaji wa adhabu kwa kila mwezi au sehemu ya mwezi.wakati kushindwa kuwasilisha au kulipa kodi kunaendelea. Kiasi cha adhabu kinachukuliwa kuwa ya kiwango cha juu kama ifuatavyo;

2.5% ya kiasi cha kodi iliyokadiriwa pamoja na ritani ya kodi,kutoa kodi iliyolipwa kuanzia kipindi kwa kiwango hicho.
 Kwa watu binafsi ni pointi za sarafu 5 na kwa ajili ya Kampuni ni pointi za sarafu 15.
 

Kumbuka:
Adhabu ya uchelewaji inatekelezwa tofauti na ya kushindwa kuwasilisha makadirio/ritani ya awali na kushindwa kuwasilisha ritani ya mwisho.
 

3.Adhabu kwa kutoa taarifa zisizo za ukweli au upotoshaji.
 

Taarifa zisizo za ukweli au zinazopotosha ambazo matokeo yake ni ulipaji wa kodi usio sahihi unapelekea kutozwa adhabu.
Na adhabu ni kama ifuatavyo:-
 

  • Taarifa au kamisheni itakayopatikana bila sababu za udhuru itatozwa adhabu ya 50% ya kodi pungufu.
  • Taarifa au kuacha kutotoa kunakofanyika kwa kuelewa au uzembe,adhabu ni 100% ya kodi pungufu.
     

Kumbuka:
Adhabu itaongezeka kwa 10% kwa mara ya pili au kwa kurudia kwa mfuatano itapunguzwa 10%.Ikiwa mtu kwa kujitolea atatoa taarifa kabla ya kugunduliwa na
Afisa wa kodi au wakati wa ukaguzi wa kodi unafuata wa mlipakodi. Mtu atasemekana ametoa taarifa zisizo za ukweli au upotoshaji ikiwa atatoa taarifa kwa afisa wa kodi ambazo zisizo za ukweli au upotoshaji kupitia kwenye nyaraka au kuziondoa kutoka kwenye taarifa iliyotolewa kwa afisa wa kodi ,kila kitu ambacho kina taarifa ya upotoshaji katika mtu husika.
 

4.Adhabu kwa Kusaidia na Kushawishi
 

Mtu anayesaidia ,kushawishi,Kushauri,kusababisha mtu mwingine kufanya makosa kwa kuvunja vipengere vya sheria itakapothibitika,mtu huyo atatozwa adhabu ya 100% ya kodi pungufu.
 

Makosa:
Uvunjaji wa vipengere vya sheria za kodi unapelekea matokeo ya kufanya makosa .Hii inahusisha taratibu mpaka itakapothibitika kwa mtu huyo na taratibu za kukomboa kodi kwa makosa mbalimbali yaliotolewa na Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya mwaka 2015.