Emblem TRA Logo

Utangulizi:

Mwongozo huu unafafanua utozaji kodi wa makampuni; ni kwa namna gani kampuni inahitajika kutoa taarifa ya kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania. Inatoa pia mwongozo wa kina na unaohitajika.

 

Nini maana ya kodi ya makampuni?

Kodi ya makampuni ni kodi inayotozwa katika mapato yanayotozwa kodi (Faida) ya asasi kama vile makampuni yenye dhima ya ukomo na makampuni mengine ikiwa ni pamoja vilabu, vyama, jumuiya na vikundi vingine visivyo shirikishi.

 

Mwongozo huu unatoa mtazamo wa msingi wa kodi ya Makampuni. Unaelezea maana ya “kodi ya makampuni” nani anawajibika na anapaswa kufanya nini na lini ikiwa atatakiwa kutimiza masharti ya Kodi ya makampuni. Unabainisha namna kodi inavyokokotolewa, viwango vya kodi vinavyohusika na muda wa kulipa.

 

Unaelezea pia dhana za msingi zinazohusiana na kodi ya mapato kama vile “makadirio binafsi”, “ muda wa kufanya mahesabu” na “ Faida inayolipiwa kodi”

 

Kodi ya makampuni ni kodi inayotozwa katika mapato yanayotozwa kodi (faida) ya asasi kama vile makampuni yenye dhima ya ukomo, taasisi, au makampuni ikiwa ni pamoja na klabu, vyama, jumuiya, ushirika, mashirika ya wahisani na vikundi vingine visivyo shirikishi.

 

Mapato yanayotozwa kodi (faida) katika kodi ya makampuni yanahusisha:

 

Faida inayotokana na shughuli za biashara

Faida kutokana na uwekezaji (isipokuwa migawanyo ya faida ambayo imetozwa kodi tofauti kama kodi ya mwisho)

Kodi inayotokana na mapato ya makampuni yenye hasara za muda mrefu ambazo hazijasamehewa  kwa miaka mitatu mfululizo.

Ni nani wanapaswa kulipa kodi ya Makampuni?

a)    Makampuni yenye dhima ya ukomo

 

b)    Amana

 

c)    klabu

 

d)    Asasi zisizo za Kiserikali

 

e)    vyama vya ushirika

 

f)    Mashirika ya Wahisani

 

g)    Makampuni ya ndani ya kudumu (Matawi ya makampuni ya nje)

 

h)    Vyama vya siasa

 

i)     Wakala wa serikali

 

j)   Kampuni mpya iliyoanzishwa na ambayo inajihusisha na utengenezaji wa madawa ya binadamu na bidhaa za ngozi na ina mkataba wa makubaliano na Serikali ya Jamhuli ya Muungano wa Tanzania itatozwa kodi kwa kiwango cha 20% kwa kipindi cha miaka mitano mfulizo kutoka mwaka walipoanza uzalishaji

Je Wabia wanapaswa kulipa kodi ya Makampuni ?

Wabia hawalazimiki kulipa kodi ya mapato. Hata hivyo, wabia wanatozwa kodi ya mapato katika faida zinazosambazwa kutoka kwenye ubia kwa kuzingatia uwiano wa uchangiaji

Nini maana ya mwaka wa mapato?

Katika muktadha wa kodi ya mapato, mwaka wa mapato una maana ya kalenda ya mwaka wa miezi kumi na miwili (kwa maana ya kipindi kinachoanzia tarehe 1 Januari hadi tarehe 31 Desemba). Hata hivyo, Asasi inaweza kuomba kwa maandishi kwa Kamishna kibali cha kubadili mwaka wake wa mapato kutoka mwaka unaoanzia Januari kwenda mwaka unaoanzia wakati mwingine unaopendekezwa na asasi. Mwaka wa mapato ni muhimu katika utunzaji wa hesabu za kodi. 

Nini maana ya taarifa ya mapato ya kodi?

Taarifa ya mapato ni maelezo yanayowasilishwa Mamlaka ya Mapato Tanzania yanayoonesha makadirio ya mapato na kodi inayolipwa au mapato ya mwisho na kodi inayolipwa kwa kila mwaka wa mapato.

 

Chini ya sheria ya kodi ya mapato, kampuni inatakiwa kuwasilisha taarifa ya mapato hata kama hakuna mapato yanayotozwa kodi.

Maelezo kuhusu makadirio ya kodi inayolipwa

Kila kampuni iliyosajiliwa na watu binafsi ambao wanapaswa kuandaa hesabu za mizania na kuwasilisha taarifa inayoonesha makadirio ya kodi inayolipwa katika kila mwaka wa mapato.

 

Maelezo ya makadirio/makadirio yaliyopitiwa upya ya kodi inayolipwa kwa awamu kwa niaba ya kampuni.

 

 

Maelezo ya makadirio/makadirio yaliyopitiwa upya ya kodi inayolipwa kwa awamu na mtu binafsi

 

Tarehe ya mwisho (makataa) ya kulipa kodi

 

Taarifa ya makadirio ya kodi inayolipwa yanapaswa kuwasilishwa ofisi za TRA katika tarehe zifuatazo kutegemeana na muda wa mahesabu:

 

i.             Ifikapo au kabla ya tarehe 31 Machi

 

ii.            Ifikapo au kabla ya tarehe 30 Juni

 

iii.           Ifikapo au kabla ya tarehe 30 Septemba

 

iv.           Ifikapo au kabla ya tarehe 31 Desemba

 

Malipo ya awamu ya kwanza ya kodi yanaishia wakati taarifa ya makadirio ya kodi inayolipwa (taarifa ya awali ya mapato) inapowasilishwa na kisha awamu nyingine zitalipwa kwa kuzingatia tarehe za makataa zilizoainishwa hapo juu.

 

 

Ucheleweshaji wa malipo ya kodi:Atatozwa riba kwa kiwango cha kisheria kinachojumuishwa kila mwezi italipwa kwa Kamishna Mkuu.

Taarifa ya mwisho ya mapato:

Taarifa ya mwisho ya mapato inapaswa kuwasilishwa ndani ya miezi sita kuanzia mwisho wa tarehe ya hesabu. Taarifa hii inapaswa kuandaliwa au kuthibitishwa na Mhasibu ambaye amethibitishwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu


 

Tarehe ya mwisho ya kodi ya kujitathmini

Tarehe ya mwisho ya malipo ya kodi kulingana na marejesho (kodi ya mwisho uliojitathmini) ndio tarehe inayotarajiwa ya kuwasilisha marejesho.