Uwanda wa wazi Ni eneo la forodha ambalo mtu anaruhusiwa kuingiza nchini mitambo, mashine, vifaa na malighafi bila kulipa ushuru wa forodha kwa ajili ya utengenezaji bidhaa za kuuza nje ya nchi. Muagizaji wa bidhaa hiyo huweka dhamana ili kuingiza mzigo huo. Bidhaa iliyoingizwa iko chini ya udhibiti wa forodha katika uingizaji, kupitia mchakato wa utengenezaji, hadi wakati wa uuzaji/usafirishaji (nje ya nchi) au malipo ya ushuru kama bidhaa zilizotengenezwa zitauzwa nchini.
Faida zingine za kuendesha biashara hizo ni pamoja na; kufanya biashara bila kodi yeyote, taratibu zilizorahisishwa zaidi katika kusajili na kupata leseni na uwezo wa kufanya biashara kwa muda mrefu bila kulipa kodi.
Ni taasis ipi inayohusika na kusajili Uwanda wa wazi (EPZ)
Mtu anaetaka kuanzisha uwanda wa wazi (EPZs) anaweza kupata leseni kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara
Ni taratibu zipi za kufuata kuingiza bidhaa chini ya Uwanda wa Wazi (Reg. 169)
Muingizaji atapaswa:
Kutoa tamko la kuingiza bidhaa kupitia fomu namba C.17 na kutekeleza matakwa ya thamana kwa kutumia fomu CB. Thamana inayowekwa ni mbadala wa kodi ambayo ingelipwa wakati wa kuingiza bidhaa nchini. Pia dhamana hiyo inalinda kodi ya serikali iwapo bidhaa zilizoingia zitatumika kwa malengo mengine na kuingizwa kwenye soko la ndani.
Kuwasilisha bidhaa zilizoingia pamoja na fomu namba C.17 kwa afisa wa forodha anaehusika na Uwanda wa wazi kwa ajili ya kuzipokea na kutunza kumbukumbu
Kutua sehemu maalum kwa ajili ya ukaguzi ndani ya Uwanda wa Wazi ambapo bidhaa zinazoingia nchini zinakaguliwa or kuhakikiwa. Kamishna kwa sababu za msingi anaweza kumuagiza afisa wa forodha kufanya ukaguzi wa bidhaa pale inapoingia tu nchini.
Nani anayetunza kumbukumbu za bidhaa zinazoingia au kutoka Uwanda wa Wazi
Mmiliki wa Uwanda wa Wazi atapaswa kutunza kumbukumbu za shehena ya malighafi na bidhaa katika kitabu cha usajili cha kila mwezi na kukitoa kwa afisa wa forodha kwa ajili ya ukaguzi kabla ya siku 15 ya mwezi unaofuata mwezi wa biashara
Endapo katika ukaguzi, bidhaa zimepungua kulinganisha na idadi iliyoingizwa, mwendeshaji wa Uwanda wa Wazi atapaswa kulipa adhabu ambayo ni sawa na mara mbili ya kodi inayopaswa kulipwa
Taratibu za kuondosha bidhaa nchini zinazopaswa kufuatwa na Muendeshaji wa Uwanda wa Wazi (Kanuni.171)
Bidhaa zilizokusudiwa kuuzwa nje ya nchi, chini ya uwanda wa wazi, lazima malighafi ziingizwe nchini kwa kutumia fomu namba C.17
Dhamana kwa ajili ya kuondosha bidhaa kutoka Uwanda wa Wazi kwenda bandarini kwa ajili ya usafirishaji kwenda nje ya nchi itatekelezwa kwa kutumia fomu CB.
Bidhaa pamoja na nakala ya uondoshaji bidhaa itapelekwa katika bandari ya uondoshaji.
Kama lakiri iliyowekwa na afisa wa Uwanda wa Wazi umeondolewa au kuchezewa kwa namna yeyote, ukaguzi utafanywa tena na afisa wa forodha mpakani
Nakala iliyodhibitishwa ya fomu C17 inayohakikisha kuwa uondoshwaji wa bidhaa kwenda nje ya nchi umefanyika, itapewa kwa mmiliki kwa ajili ya kuondosha dhamana (bond cancellation)
Taratibu za kufuata unapohamisha bidhaa kutoka Uwanda Wazi kwenda mwingine
Ingiza bidhaa kutoka Uwanda wa Wazi kwenda mwingine kwa kutumia fomu C17
Tengeneza dhamana ya kutoa mzigo kutoka Uwanda wa Wazi kwenda mwingine kwa kutumia fomu CB
Chukua nakala ya fomu C17 iliyohakikiwa kutoka kwa afisa wa Uwanda wa Wazi unaopokea bidhaa kwa ajili ya kufuta dhamana (CB)
Kama bidhaa zitahamishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine ndani ya uwanda wa wazi, Kiongozi wa Kampuni lazima amtaarifu afisa wa forodha.
Utekelezaji wa dhamana ya forodha (CB)
Je ni taratibu zipi za kufuata unapohamisha mitambo na mashine kutoka Uwanda wa Wazi kwenda eneo lingine (Kanuni ya 173)
Mitambo, Mashine na vifaa vinaweza kutolewa kwa ajili ya ukarabati na matengenezo kutoka Uwanda wa Wazi kwenda eneo la forodha itaambatana na utaratibu wa forodha wa kuingiza bidhaa nchini kwa kutumia fomu C17
Fomu inayotumika kutoa dhamana ya mitambo, mashine na vifaa ni fomu CB.
Ni taratibu zipi zinazotumika kutupa na kuteketeza taka?
Kutupa na kuteketeza takataka kunaweza kufanyika ndani ya Uwanda wa Wazi chini ya Afisa wa forodha. Cheti cha kuteketeza na kuharibu taka hizo kitatolewa na Afisa wa Forodha.
Taratibu za kawaida za forodha za kuingiza bidhaa zitatumika pale ambapo taka zitaingizwa kwenye soko la ndani.
Je kuna taratibu maalum wakati wa kusafirisha bidhaa za Uwanda wa Wazi?
Bidhaa zinazosafirishwa kwenda/kutoka uwanda wazi zinatakiwa zisafirishwe kwenye magari yenye “lakiri,isipokuwa kwa bidhaa zenye maumbo makubwa ambazo ni lazima zipate kibali cha Kamishna.Bidhaa ndogondogo zinatakiwa kusafirishwa kwenye masanduku ya chuma ambayo yana “lakiri” ya forodha.
Habari & Matukio
Ufanisi wa Bandari umeongeza mapato ya Serikali
Mwenyekiti wa Bodi aonyesha njia TRA kuvuka malengo