Emblem TRA Logo
Taratibu za kuondosha Bidhaa nchini

Utangulizi

Mahuruji ina maana kuchukua au kusababisha bidhaa kusafirishwa nje ya Tanzania. Mahuruji husafirishwa bila kutozwa ushuru na kodi isipokuwa kwa vipengele vitatu; Ngozi ghafi ambazo zinabadilishwa kwa kiwango cha 80% ya thamani ya Bei Bila Usafiri au dola za Marekani 0.52 kwa kg yoyote iliyo kubwa Zaidi, Viwango hivi havitatozwa kwa wawekezaji waliosajiliwa chini ya EPZ ambao wana cheti cha kuchakata nyama. Korosho ghafi ambazo zinatozwa kiwango cha 15% ikikokotolewa katika Bei Bila Usafiri au Dola za Marekani 160 kwa tani ya ujazo yoyote iliyo kubwa Zaidi, na ngozi chepe zinatozwa kiwango cha 10% ya thamani ya bei bila usafiri.

Nitashughulikia vipi nyaraka za mahuruji?

  • Msafirishaji wa bidhaa nje ya nchi anatakiwa kumteua Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo atakayeshughulikia nyaraka zake za kusafirisha nje bidhaa.
  • Mchakato wa maandalizi ya nyaraka hufanyika mtandaoni na kukamilika kabla ya ukaguzi wa mizigo na kutoa kibali cha kusafirisha bidhaa nje ya nchi.
  • Mchakato wa awali huanza kwa msafirishaji mzigo nje ya nchi kumteua Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo
  • Msafirishaji Bidhaa nje ya nchi anamkabidhi Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo nyaraka kwa mkono au kielektroniki ambaye anazipakia kwenye Mfumo wa Pamoja wa Forodha Tanzania (TANCIS) kwa Tanzania bara na mfumo wa ASYCUDA++ kwa upande wa Zanzibar pamoja na viambatisho vyote vya nyaraka husika ikiwa ni pamoja na vibali kutoka Idara Nyingine za Serikali kwenda TRA. Idara Nyingine za Serikali zinahakiki kibali kama kipo (inakataa au kuthibitisha).
  • Ukadiriaji wa kodi na ushuru wa kusafirisha mizigo nje ya nchi kama upo.
  • Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo ataagiza kontena kutoka kampuni/wakala wa usafirishaji kwa meli.
  • Atapanga mzigo wa kusafirisha nje kwenye kontena chini ya usimamizi wa TRA na Idara Nyingine za Serikali.
  • Kampuni/Wakala wa Usafirishaji kwa Meli atawasilisha TRA taarifa za ratiba ya chombo kinachosafirisha bidhaa hiyo nje ya nchi.
  • TRA itakagua (kuidhinisha/kukataa) tamko la kupakia mzigo (tamko la kupakia mzigo lililothibitishwa litapelekwa moja kwa moja kwa msimamizi wa Kituo kama Orodha ya Kupakia Mzigo na kutarajiwa kuingizwa chomboni).
  • Ukaguzi Langoni kulingana na lango la kituo cha TRA.
  • Kituo kinawasilisha ripoti ya Kuingiza Mzigo kwenda TRA ili kuthibitisha kuwasili kituoni kwa mzigo wa kusafirishwa nje ya nchi.
  • Ripoti ya matokeo ya Kupakia (mzigo mdogo/wa kawaida uliopakizwa) inawasilishwa na kituo TRA.
  • Ripoti ya kupakia mzigo kwa kufuata utaratibu wa TRA.
  • Kuwasilisha orodha ya shehena ya kusafirishwa nje inayotolewa na Kampuni/Wakala wa Meli kwenda TRA.
  • TRA Inakagua (inaidhinisha) orodha ya shehena ya kusafirishwa nje (kwa kukata moja baada ya nyingine katika orodha inayotoka kituoni)

Angalizo:

  • Kwa Msafirishaji wa mizigo kutoka Zanzibar anampatia Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo nyaraka kwa mkono au kielektroniki ambaye anazipakia kwenye Mfumo wa Kikompyuta wa kuingiza Data za Forodha (ASYCUDA++) na kuingiza nyaraka hizohizo TRA; ambapo namba ya kumbukumbu inatolewa moja kwa moja.
  • Msafirishaji bidhaa nje ya nchi ataijulisha idara ya forodha kabla ya kupakia mzigo kwenye kontena au gari la mizigo kwa kuwa afisa wa forodha atatakiwa kushuhudia mchakato wa kupakia mzigo
  • Kuwekesha nafasi katika usafirishaji wa melini hauitajiki kama mzigo unapitia kwa njia ya barabara.

Nyaraka gani zinahitajika?

Nyaraka zifuatazo zitatolewa kwa ajili ya kusafirisha mzigo nje ya nchi:

  • Ankara
  • Orodha ya kufungashia
  • Hati ya TIN (msafirishaji nje)
  • Barua ya kuidhinisha
  • Hati za kusafirisha nje bidhaa kutoka Mamlaka husika kutegemea aina ya mzigo utakaosafirishwa nje; hati hizi ni pamoja na:
  1. Hati kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa
  2. Hati kutoka Wizara ya Kilimo na Chakula
  3. Hati kutoka Wizara ya Nishati na Madini
  4. Hati kutoka Wizara ya Maliasili

Taarifa kuhusu Fedha Taslimu na Hati za Malipo zinazosafirishwa kuingia au kutoka nje ya Nchi