Hii ni kodi inayotozwa kwenye mapato yatokanayo na michezo ya kubahatisha. Kodi hizi ni za aina mbili: -
- Kodi ya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Tax)
Hii ni kodi anayotozwa mwendeshaji wa mchezo wa kubahatisha kutokana na mapato yake yatokanayo na michezo ya kubahatisha.
- Kodi ya Michezo ya Kubahatisha kwenye Zawadi (Gaming Tax on Winnings)
Hii ni kodi anayotozwa mchezaji baada ya kushinda zawadi ya mchezo wa kubahatisha.
Aina ya michezo inayotozwa kodi hii: -
(a) Kasino (Casino)
(b) Kasino Mtandao
(c) Kasino ndogo (Mini Casino/Forty machines sites)
(d) Michezo ya Kubashiri Matokeo (Sports Betting),
(e) Michezo ya Machine (Slots machines/route operations),
(f) Bahati Nasibu ya Taifa (National lottery)
(g) Bahati nasibu ya kutumia ujumbe mfupi wa simu.(SMS lottery)
(h) Michezo ya Vikaragosi (Virtual Games)
Walipakodi katika Tasnia ya michezo ya kubahatisha wanaelekezwa yafuatayo:
(a) Kulipa kodi zitokanazo na michezo ya kubahatisha kwa viwango vilivyowekwa
(b) Kujisajili na kutapata Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi kama hawajasajiliwa.
(c) Kujaza na kuwasilisha ritani za kodi za michezo ya kubahatisha katika ofisi za TRA amabazo wamesajiliwa.
(d) Kujaza GFS sahihi kama zilivyoonyeshwa hapo juu wakati wa kufanya malipo ya kodi ya michezo ya kubahatisha kwa kadri ya mchezo wa kubahatisha ulihusika.
Angalizo:
Vipengele vya Sheria ya Usimamizi wa Kodi kuhusiana na kutunza kumbukumbu, madeni ya kodi, kukusanya na kukomboa kodi, kutoza riba na pingamizi za kodi vitahusika pia katika kutoza na kusimamia kodi ya michezo ya kubahatisha.
Viwango vya kodi vinavyotozwa na tarehe ya kulipa kodi
Kodi ya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Tax);
Na | Aina ya Mchezo | Viwango vya kodi vinavyotozwa | Tarehe ya kulipa kodi |
1 | Kasino (Land Based Casino) | 18% ya Mapato Ghafi (mauzo baada ya kutoa gharama za ushindi) 12% ya Jumla ya zawadi aliyoshinda Mchezaji | Kila wiki |
2 | Kasino Mtandao (Internet Casino) | 25% ya Mapato Ghafi (Mauzo baada ya kutoa gharama za ushindi) 15% ya Jumla ya zawadi aliyoshinda Mchezaji
| Kila Mwezi |
3 | Michezo ya Kubashiri Matokeo (Sports Betting) | 25% ya Mapato Ghafi (Mauzo baada ya kutoa gharama za ushindi) 10% ya Jumla ya zawadi aliyoshinda Mchezaji
| Kila mwezi |
4 | Bahati nasibu ya kutumia ujumbe mfupi wa simu (SMS Lotteries) | 25% ya Mapato Ghafi (Mauzo baada ya kutoa gharama za ushindi) 15% ya Jumla ya zawadi aliyoshinda Mchezaji
| Kila mwezi |
5 | Bahati Nasibu ya Taifa (National Lotteries) | 20% ya Mapato Ghafi (Mauzo baada ya kutoa gharama za ushindi) 15% ya Jumla ya zawadi aliyoshinda Mchezaji
| Kila mwezi |
6 | Kasino ndogo (Forty Machines Sites) | 25% ya Mapato Ghafi ya Michezo ya Kwenye Mashine (Mauzo baada ya kutoa gharama za ushindi)
| Kila mwezi |
7 | Michezo ya Machine (Slot Machines) | Tshs. 100,000 kwa kila mashine | Kila mwezi |
8 | Michezo ya Vikaragosi(Virtual Games) | 10% ya jumla ya zawadi anayopata Mchezeshaji 15% ya jumla ya zawadi aliyoshinda Mchezaji | Kila mwezi
|
Takwimu za Fedha za Serikali na Maelezo
Kifungu Namba ya Takwimu ya Fedha ya Serikali Maelezo 440 11440107 Michezo ya Kubashiri Matokeo kwenye mapato ghafi 440 11440108 Michezo ya Kubashiri kwa wachezaji 440 11440109 Michezo ya mashine 440 11440110 Bahati Nasibu ya kutumia ujumbe mfupi wa simu 440 11440111 Bahati Nasibu ya Taifa 440 11440112 Mapato ghafi kwenye Kasino 440 11440113 Zawadi anayopata Mchezaji 440 11440114 Kasino Ndogo 440 11440115 Michezo ya Vikaragosi kwa Mchezeshaji 440 11440116 Mchezo wa Vikaragosi kwenye zawadi anayopata Mchezaji
Habari & Matukio
Ufanisi wa Bandari umeongeza mapato ya Serikali
Mwenyekiti wa Bodi aonyesha njia TRA kuvuka malengo