Nani anastahili kuwa Mkazi anayerejea nchini?
Huyo ni mtu anayewasili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania ambapo ofisa anayehusika ameridhika kuwa kiuhalisia anabadili ukazi kutoka nje ya Tanzania na kwenda mahali fulani nchini Tanzania; ambapo mtu huyo hajawahi kupata msamaha wa kodi au hakuishi Tanzania kabla ya kuwasili kwake zaidi ya ziara za muda akiwa si mkazi.
Je, kuna makataa ya muda wa kuingiza mizigo yangu nchini kama mkazi anayerejea nchini?
Msamaha wa kodi utatolewa kwa mkazi aliyerejea nchini kwa mizigo aliyoiingiza nchini kutoka nje ya nchi ndani ya siku 90 tangu tarehe ya kuingia kwake au muda zaidi usiozidi siku 360 kutoka siku aliyoingia nchini kadiri Kamishna atakavyoruhusu.
Angalizo: Uingizaji wa bidhaa bila ushuru kwa mujibu wa sheria hautaruhusiwa kama zitaingizwa bila kuandamana na mhusika.
Mizigo gani Inaruhusiwa kuingizwa nchini bila kodi?
Mizigo ifuatayo inaruhusiwa inapoingizwa nchini kama mizigo ya mkazi anayerejea nchini ambaye amefikia umri wa miaka 18:
(a) mavazi;
(b) Vifaa binafsi na vya nyumbani vya aina yoyote ambavyo alikuwa anatumia binafsi au katika makazi yake ya awali;
(c) Chombo cha moto,"(ukiondoa mabasi na mabasi madogo yenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 13 na magari ya mizigo yenye uwezo wa kubeba mzigo zaidi ya tani mbili. Aidha, chombo hicho cha moto kisiwe kimetumika miaka 8 au zaidi tangu kilipotengenezwa na kiwe na ukubwa wa injini usiozidi cc 3000) na kimemilikiwa binafsi na msafiri huyo na amekitumia nje ya Tanzania kwa takriban miezi 12 (ukiondoa kipindi cha usafirishaji hususani kama kilisafirishwa kwa meli).
Habari & Matukio
Ufanisi wa Bandari umeongeza mapato ya Serikali
Mwenyekiti wa Bodi aonyesha njia TRA kuvuka malengo