KUANZISHA BIASHARA
Katika kurasa hii utaona miongozo itakayokuongoza kuhusu mambo ya msingi unayohitaji kufanya wakati unapoanzisha biashara kama mtu binafsi, ubia, amana au kampuni yenye dhima ya ukomo
Unatakiwa kufanya nini unapotaka kuanzisha biashara?
Mtu Binafsi
Mtu awe mkazi au asiye mkazi anatakiwa kutembelea tovuti yetu www.tra.go.tz ili kupata TIN (Nambari ya Utambulisho wa Mlipakodi). Ataombwa kujaza fomu ya maombi ya TIN Mtandaoni kupitia https://taxpayerportal.tra.go.tz tovuti ya mlipakodi na ataongozwa juu ya hatua za kufuata juu ya kujibu maswali ya mtandaoni na kuweka viambatisho vinavyohitajika, Baada ya hii Kwa madhumuni ya Tin ya biashara. mtu binafsi anatakiwa kutembelea ofisi zetu akiwa na barua kutoka kwa kiongozi wa serikali ya mtaa na mkataba wa pango mahali anapofanyia biashara. Baada ya kupewa cheti cha TIN, Mlipakodi atatakiwa kufanyiwa makadirio ya kodi kwa ajili ya tathmini ya kodi na baada ya kutimiza mipango/taratibu za kodi, Mlipakodi atapewa Cheti safi cha kodi ili kuwezesha kupata Leseni ya Biashara kutoka Ofisi ya Biashara katika Wilaya, Manispaa, Jiji na Wizara ya Biashara. na Viwanda kulingana na aina ya biashara.
Mkazi ni Nani?
Mtu anastahili kuwa mkazi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa:-
- Atakuwa na makazi ya kudumu katika Jamhuri ya Muungano na atakuwepo wakati wowote katika kipindi cha mwaka wa mapato.
- Yupo katika Jamhuri ya Muungano katika mwaka wa mapato kwa kipindi au vipindi vinavyofikisha jumla ya siku 183 au zaidi.
- Yupo katika Jamhuri ya Muungano katika mwaka wa mapato na kila moja ya miaka miwili iliyotangulia ya mapato kwa vipindi vinavyofikia wastani wa siku 122 katika kila moja ya mwaka huo wa mapato.
- Ni mwajiriwa au ofisa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano aliyepangiwa kazi nje ya nchi katika mwaka wa mapato.
Hati ya Usajili:
Mtu binafsi anaweza kuamua kusajili jina la biashara kwa wakala aliyepewa kazi hiyo na Wizara ya Biashara na Viwanda anayejulikana kama Mamlaka ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). Jina lililosajiliwa linaweza kupatikana kabla au baada ya kufanya maombi ya TIN. Jina la biashara lililosajiliwa litaonyeshwa kwenye hati ya TIN pamoja na jina la mtu huyo ikionyesha jina la mmiliki wa biashara kama (T/A).
Shirika (kampuni yenye dhima ya ukomo)
Kuanzisha shirika kunahitaji mtu aombe kupatiwa Hati ya shirika kutoka Mamlaka ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). Wahamasishaji wa kampuni wanatakiwa kuandaa na kuwasilisha hati na Mkataba na kanuni za kampuni.
Hati ya usajili wa shirika iambatishwe kwenye maombi ya TIN pamoja na Mkataba na Kanuni za Kampuni wakati mtu anapopeleka maombi TRA.
Kampuni yenye dhima ya ukomo itaomba kupatiwa hati ya TIN kwa kujaza fomu za maombi kama ifuatavyo:
- Maombi kwa ajili ya kampuni.
- Maombi kwa ajili ya wanahisa/wakurugenzi, iwapo mkurugenzi yeyote kati yao ameshapatiwa hati ya TIN kwa madhumuni mengine anaweza kutoa maombi mengine. Namba ileile ya TIN itatumika.
- Kwa wakurugenzi ambao si raia wanapaswa kutimiza masharti yote ya uhamiaji na kupata kibali cha biashara kutoka Idara ya Uhamiaji inayofanya kazi chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
Ubia
Wabia wanatakiwa kusajili kampuni katika ofisi za BRELA na kupata hati ya usajili ambayo inaonyesha namba na majina ya wabia pamoja na mgawanyo wa hisa zao.
- Katika kutoa maombi ya TIN kampuni ya ubia itaomba kupatiwa hati kwa kuwasilisha nakala ya usajili waliyopata BRELA.
- Kila mbia ataomba kupatiwa TIN, iwapo mbia yeyote tayari ameshapatiwa hati ya TIN kwa madhumuni mengine hatakiwi kutoa maombi mengine. Namba ileile ya TIN itatumika.
Udhamini
Udhamini ni mpango ambapo wadhamini wanamiliki mali lakini haihusishi ubia na kampuni.
Amana inapaswa kusajiliwa kama kampuni katika ofisi za BRELA na kupata hati ya usajili ambayo inaonesha majina na anwani za wadhamini. Kila mdhamini anapaswa kuomba kupatiwa hati ya TIN, iwapo mdhamini yeyote kati yao akiwa ameshapatiwa hati ya TIN kwa madhumuni mengine hawezi kutuma maombi mengine. Namba ya TIN aliyo nayo itatumika.
Shirika la msaada:
Shirika hili litatambulika kama shirika la msaada kwa madhumuni ya masuala ya kodi baada ya kupatiwa kibali na Kamishna Mkuu. Mwombaji anatakiwa kupata nyaraka zote muhimu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani.
Tamko la Makadirio ya Mapato
Utatakiwa kutoa tamko la makadirio ya mapato kwa ajili ya kufanyiwa makadirio ya awali ya kodi kwa mwaka husika. Afisa wa kodi anaweza kukuhoji na kurekodi taarifa za biashara yako na taarifa zako binafsi katika ofisi ya TRA.
Habari & Matukio
Ufanisi wa Bandari umeongeza mapato ya Serikali
Mwenyekiti wa Bodi aonyesha njia TRA kuvuka malengo