Emblem TRA Logo

Naibu Kamishna Mkuu Tra Ashiriki Warsha Ya Wataalamu Na Watafiti Wa Masuala Ya Uchumi Na Kodi

01 April, 2024

Featured Image

 

Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Mcha Hassan Mcha ameshiriki katika ufunguzi wa Warsha ya siku mbili inayowakutanisha wataalamu na watafiti wa masuala  ya Uchumi na kodi kutoka nchi mbali mbali Duniani kujadili Umuhimu wa Kodi katika ukuaji  wa uchumi wa nchi zinazoendelea  kupitia Kodi. 

Warsha hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Ukuaji wa Uchumi wa Kimataifa (IGC) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Taasisi ya Utafiti wa kupambana na Umasikini (REPOA) ilifunguliwa na Kamishna wa Fedha za Nje, Bw. Rished Bade kwa niamba ya waziri wa Fedha leo tarehe 15. 05. 2024, jijini Dar es Salaam.