Emblem TRA Logo
Mapato ya uwekezaji raslimali

Faida ya mtaji kutokana na kupata riba katika ardhi na majengo.

 Upatikanaji wa riba katika ardhi na majengo

 

Mtu anayepata riba katika ardhi au jengo  atachukuliwa kama anapata mali pindi atakapoacha kupata riba hiyo ikiwa ni pamoja na wakati mali hiyo inapouzwa, inapobadilishwa, inapobadilishwa umiliki, inapogawanywa, inapobatilishwa, inapokombolewa, inapoteketezwa, au inaposalimishwa na katika suala la riba ya mali hiyo uwepo wake unapokoma, mara kabla ya kuwepo ukomo wa mali hiyo.

Sheria ya Kodi ya Mapato inamtaka mtu anayepata faida kutokana na kupata riba katika ardhi au majengo yaliyo katika Jamhuri ya Muungano, kulipa kodi ya mapato kwa awamu moja.

Awamu Moja ya Malipo ni nini?

Kodi ya mapato inayolipwa kwa awamu moja kutokana na kupata riba katika ardhi au majengo ni kiasi cha kodi kinacholipwa mara moja kabla umiliki haujahamishwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine. Msajili wa Hatimiliki hatasajili uhamishaji huo pasipo kuonyesha hati kutoka Mamlaka ya Mapato inayothibitisha kuwa malipo ya awamu moja yamelipwa au hayalipwi. Muuzaji anatakiwa kutoa taarifa kuhusu uhamishaji wa riba ya ardhi au jengo kwa kujaza fomu: # ITX 204.01.E

Viwango Vinavyotumika

(a)      10% ya faida kwa mkazi;

(b)      20% ya faida kwa mtu asiyekuwa mkazi

Hata hivyo, Sheria Kodi ya Mapato inaeleza kuwa mlipaji kwa awamu atastahili punguzo la kodi kwa mwaka wa mapato wa kiasi sawa na kodi ya mapato iliyolipwa kwa awamu moja kwa mwaka wa mapato.

 

Misamaha ya Kodi

 a)   Iwapo makazi yamekuwa yakimilikiwa mfululizo na mtu kwa miaka mitatu au zaidi na mtu huyo amekuwa akiishi humo mfululizo au kwa vipindi vya jumla ya miaka mitatu au zaidi; na riba ilipatikana kwa faida isiyozidi ShT 15,000,000

b)  Riba katika ardhi inayomilikiwa na mtu yenye thamani ya soko ambayo ni pungufu ya ShT 10,000,000 wakati ilipopatikana na imekuwa ikitumika kwa madhumuni ya kilimo kwa angalau miaka miwili kati ya mitatu kabla ya kupatikana.

c) Hisa Hisa zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa la Dar-es- Salaam zinazomilikiwa na mkazi au asiye mkazi kwa kiwango kisichozidi 25%.

d)Mapato Kutokana na kuhamisha umiliki au hisa au taarifa za madini kwa Wabia ambao ni Kampuni na Serikali

Faida itokanayo na uuzaji wa rasilimali Inakokotolewaje?

Mapato yanayotokana na rasilimali ya majengo na ardhi yanakokotolewa kama ifuatavyo:

Thamani ya makadirio iliyopokelewa au iliyoongezeka kutokana na kupatikana kwa riba katika ardhi au majengo

toa gharama za ununuzi

toa matumizi yaliyotumika katika maboresho yoyote ya mali

toa  matumizi yaliyotumika  kwa ujumla na  kipekee katika upatikanaji wa faida.

Je, matumizi ya utekelezaji ni nini?

Haya ni matumizi yaliyofanywa kikamilifu na kwa upekee kuhusiana na utekelezaji wa maslahi katika ardhi na jengo, kama vile ushuru wa stempu, gharama za usajili, ada za kisheria na udalali. Kodi ya faida ya mtaji katika kesi ya makampuni Mapato yanayotokana na makampuni kama walipaji wa awamu moja yatatozwa ushuru kwa kiwango cha ushuru wa shirika, ambacho kwa sasa ni 30%.

KUMBUKA

Kifungu cha 90(1) cha Sheria ya Kodi ya Mapato, (Sura ya 332), kimeleta aya mpya (b) ili kutoza mtaji faida kwa kiwango cha 3% ya mapato au thamani iliyoidhinishwa ya Ardhi au Majengo, kwa wauzaji. ambao hawana ushahidi wa hati kuthibitisha gharama ya mali.

Kodi ya Faida ya Mtaji katika Upatikanaji (Uuzaji) wa Dhamana

Dhamana ni nini?

Ni  mali yoyote inayouzika  (mali za uwekezaji za aina yoyote). Dhamana kwa ujumla zimegawanyika katika makundi yafuatayo:

  • Dhamana za hisa zisizo za kudumu (k.m. Hisa za kawaida na hisa maalum za upendeleo)
  • Dhamana za madeni, (k.m. dhamana na hati za kurejeshewa malipo)
  • Dhamana   zilizozalishwa (k.m., Mkataba wa kibiashara kwa mauzo ya baadae, Mkataba wa kuuza mali kwa bei ya makubaliano kwa kuwasilisha na kulipwa baadaye, Mkataba wa mauziano usiokuwa na masharti na Biashara ya mali kwa mali).

 

Kodi ya Faida Halisi  Itokanayo na Kuuza Dhamana

Faida halisi itokanayo  na kuuza  dhamana inachukuliwa kama mapato ya uwekezaji yatakayojumuishwa katika kujua jumla ya mapato ya mtu katika mwaka wa mapato kama inavyoelekezwa na Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004. Mapato ya jumla ya asasi yanakokotolewa katika kiwango cha 30% ilhali viwango vya kodi kwa mkazi vitahusika katika mapato ya jumla ya mkazi mmojammoja.

Jumla ya mapato ni jumla ya mapato ya uwekezaji, mapato ya biashara na mapato ya ajira.

Faida Gani Zinatokana na Mauzo ya Mali za Uwekezaji?

Faida kutokanayo na mauzo ya mali ya uwekezaji ni ziada bei ya soko dhidi ya gharama ya mali hiyo.

 

Faida halisi kutokana na mauzo ya mali za uwekezaji ni jumla ya faida zote kutokana na mauzo ya mali za uwekezaji ukiondoa:-

  • Jumla ya hasara zote katika kuuza mali za uwekezaji;
  • Hasara zozote ambazo hazijapunguzwa katika kipindi cha mwaka; na
  • Hasara zozote za mwaka uliopita ambazo hazijapunguzwa.

Gharama ya mali ni nini (Dhamana)?

Gharama ya mali ni jumla ya gharama zilizotumika katika kupata mali, ikiwa ni pamoja na: 

 Dhamana Zilizoondolewa kwenye Orodha

Hisa zilizoorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam ikiwa tu hisa hizo zinamilikiwa na raia wa ndani au raia wa nje anayemiliki chini ya 25% ya hisa za kampuni husika.

 

Ukomo katika Hasara za Vitegauchumi

Iwapo mtu anapata hasarra kutokana na uwekezaji wowote inawezekana kufidia mapato kutoka kwenye uwekezaji mwingine na haiwezi kufidia mapato kutoka kwenye biashara yoyote.

Ukomo katika Faida za Mtaji

Kama mtu atapata hasara anapouza mali ya uwekezaji, inaweza kufidia faida tu kutokana na kuuza mali nyingine za uwekezaji.

Hasara za uwekezaji kutoka nje unaweza kufidia mapato ya uwekezaji toka nje tu, hasara za mauzo ya mali za uwekezaji zinaweza kufidiwa tu na mauzo ya mali za uwekezaji kutoka nje.