Utekelezaji wa Himaya Moja ya Forodha kwa Nchi wanachama
Mamlaka ya Mapato Tanzania imeshaanza kutumia Himaya moja ya forodha kwa bidhaa zinazopitia Tanzania kwenda nchi za Afrika Mashariki zenye makubaliano ya kibiashara. Awamu ya kwanza ya utaratibu huu ulizinduliwa rasmi mwezi Oktoba, 2013 kwa nchi za ukanda wa kaskazini ilijumuisha Kenya, Uganda, na Rwanda. Baada ya mafanikio kwa ukanda wa kaskazini, pia ikaanza kutekelezwa kwa ukanda wa kati ambao unajumuisha nchi za Tanzania, Burundi, Rwanda na Uganda na baadae nchi ya Sudani ya Kusini.
Himaya moja ya Forodha, faida na namna inavyofanya kazi
Himaya moja ya Forodha ni hatua ambayo itafikisha nchi wanachama wa Jumuia ya Africa Mashariki kwenye umoja wa forodha ambao kutokana na kuondoa ushuru na kanuni au kupunguza vikwazo vya forodha kwenye bidhaa zinazopita kwenye mipaka ya nchi wanachama wa jumuia wa Afrika Mashariki na hatimaye kufanya mzunguko huru wa bidhaa.
Chini ya Himaya moja ya Forodha, nchi zote wanachama: Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi Rwanda na Sudani ya Kusini zinachukuliwa kama himaya moja ya forodha ambayo maana yake ni kwamba tamko moja la forodha linafanywa katika nchi ambayo bidhaa zimepokelewa.
Tamko moja la forodha linaondoa mfumo wa zamani uliohitaji matamko mengi ya forodha ambapo bidhaa kwenda Rwanda,Burundi au Uganda zilikuwa zikihitaji mawakala wengi wa forodha,wa kwanza nchini Tanzania kwa bidhaa zinazopitia hapa nchini kwenda nje ya nchi na kwa Rwanda,Burundi au Uganda kama bidhaa zinazoingia kutoka nchi za nje,utaratibu ambao huusisha wakala wawili au zaidi wa wa kuondosha bidhaa hizo katika eneo la forodha. Faida kubwa ya mfumo huu ni kuokoa muda na Gharama.
Modus Operandi (Mfumo unavyofanya kazi)
1.0 Bidhaa ambazo asili yake ni ndani ya nchi za Afrika Mashariki
Hizi ni bidhaa ambazo asili yake ni kutoka katika nchi wanachama wa Afrika Mashariki ambazo huhamishwa kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine. Bidhaa hizi kwa sasa zitafanywa na kutolewa tamko na nchi ambayo mzigo unaenda.
Utaratibu utakaotumika kwa mzunguko usiokuwa na tozo lolote kwa bidhaa zenye asili kutoka nchi wanachama.
1.1 Tamko moja tu la forodhalitaandaliwa Tanzania na kutumika nchi zote wanachama wa Afrika Mashariki.
1.2 Ankara inapopokelewa kutoka kwa muuzaji; waingizaji wa bidhaa kupitia mawakala wao wa Forodha wanatakiwa kutoa tamko la forodha Tanzania.
1.3 Tamko la Forodha litachakatwa nchini Tanzania na malipo ya kodi yatafanyika au kuwekea mzigo dhamana ya forodha
1.4 Punde malipo ya kodi yatakapofanyika taarifa itatumwa kwa namna ya kibali cha kuondosha mzigo kwenye nchi wanachama ili kuondosha na kusafirisha bidhaa.
2.0 Bidhaa ambazo zinatoka nje ya Afrika Mashariki (Biashra ya Kimataifa)
Hizi ni bidhaa ambazo zinaingia nchi wanachama wa Afrika Mashariki kutoka kwenye masoko ya kimataifa. Bidhaa kama hizi zilikuwa zinawekwa kwenye kundi la bidhaa zinazopitia nchi moja kwenda nchi nyingine. Bidhaa hizi zinazotoka nje ya nchi wanachama wa Afrika mashariki zinafuata utaratibu ufuatao
2.1 Kibali cha uondoshaji wa mzigo kwenda Rwanda, Burundi, na Uganda hakitumiki tena, bali bidhaa hizo huchukuliwa kama bidha zilizoingia kwenye nchi husika moja kwa moja.
2.2 Kuna tamko moja tuu ambalo linapelekwa na kuchakatwa katika nchi ambayo mzigo unapokelewa kwa ajili ya kuhifadhiwa kwenye ghala la forodha,na kwa zile bidhaa zinazotumika kwenye nchi husika. Kuunganishwa kwa mifumo kumerahisisha kubadilishana taarifa, kuidhinisha malipo ya kodi na tamko la kuondosha mzigo.Mabadilishano hayo ya taarifa kati ya nchi ni muhimu kwa kuanzisha mchakato wa kuruhusu na kuondosha bidhaa kwenda katika nchi wanachana.
2.3 Bidhaa ambazo zilikuwa zinaondoshwa chini ya ghala la forodha (kutoka ghara moja kwenda ghala jingine) kwa sasa inafanyika kama ilivyoelezewa kwenye aya ya 2.2, punde ruhusa ya kuondosha bidhaa inapotolewa kutoka nchi ambayo mzigo unaenda.Mzigo utaruhusiwa kutoka chini ya mfumo wa kieletroniki wa kufuatilia bidhaa au dhamana ya kikanda (RCTG).
3.0 Bidhaa za kuuza nje kutoka EAC
Hizi ni bidhaa zinazozalishwa ndani ya Afrika Mashariki, kipindi cha nyuma zilikuwa zinahesabika kuwa ni bidhaa zinazopita kwenda nchi nyingine ndani ya nchi wanachama. Kanuni zinazotumika kwa bidhaa hizi ni: -
3.1 Usafirishaji wa bidhaa utakuwa kwa tamko moja la forodha ambalo litaandaliwa na kufanyiwa kazi kwenye nchi itakayoondosha mzigo.
3.2 Tamko la bidhaa zilizopata kibali litasambazwa kwenye mamlaka za forodha kule ambako bidhaa zinapita
3.3 Baada ya kupata kibali kuondosha mzigo, bidhaa zitawekewa lakiri ya kielektroniki na kuanza safari ya kwenda kwenye nchi itakayopokea.
3.4 Tamko litalindwa kwa dhamana ya forodha ya nchi wanachama au kusimamiwa na mfumo wa kieletroniki wa kufuatilia mzigo.
3.5 Afisa wa mpakani atathibitisha kuondoka punde mzigo unapofika, na nchi nyingine itaendelea na mchakato wa ufuatiliaji kupitia himaya.Bado mfumo haujakamilika kwenye nchi zote. Hali ya utekelezaji kwa kila nchi ni: -
· Tanzania na Rwanda
Bidhaa zote zinazoingia na kutoka Rwanda zitakuwa chini ya mfumo
· Tanzania na Burundi
Bidhaa zote zinazoingia na kutoka Burundi zitakuwa chini ya mfumo
· Tanzania na Kenya
Bidhaa zote zinazoingia na kutoka Kenya zitakuwa chini ya mfumo
· Tanzania na Uganda
Bidhaa zote zinazoingia na kutoka Kenya zitakuwa chini ya mfumo
Habari & Matukio
Ufanisi wa Bandari umeongeza mapato ya Serikali
Mwenyekiti wa Bodi aonyesha njia TRA kuvuka malengo