Utambulisho
Uingizaji bidhaa ndani ya nchi maana yake ni uingizaji wa bidhaa na huduma ziletwazo Tanzania kutoka nchi za nje. Taratibu za uingizaji bidhaa ndani ya nchi zinatakiwa zifuatwe kwa ajili ya kuondosha bidhaa katika udhibiti wa forodha kulingana na sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004.
Uingizaji wa bidhaa ndani ya nchi hapa Tanzania unafanyika kwa hatua mbalimbali ambapo Mwingizaji bidhaa anashauriwa kutoa tamko kupitia kwa wakala atakayemteua wa Kupokea na kusafirisha mizigo kwa kuwasilisha nyaraka angalau siku 7 kabla ya kuwasili kwa chombo cha usafirishaji.
Taratibu za kuchakata nyaraka za Kuingiza bidhaa nchini
- Mwingizaji bidhaa anatakiwa kumteua Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo mwenye Leseni ili aweze kupokea/kukomboa bidhaa zake.
- Orodha ya Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo
- Mchakato wa kuandikisha unafanyika mtandaoni kupitia Mfumo wa Pamoja wa Forodha Tanzania (TANCIS) kwa upande wa Tanzania bara na Zanzibar, fomu zinaweza kujazwa kabla ya bidhaa kuwasili .
- Wakala wa forodha na usafirishaji wa mizigo/waingizaji wa bidhaa wanatakiwa kujaza Tamko na makadirio binafsi kupitia Mfumo wa Pamoja wa Forodha Tanzania (TANCIS) kwa upande wa Tanzania bara na Zanzibar, na kuambatanisha nyaraka nyinginezo husika za kuingiza bidhaa/za uthibitisho angalau siku 7 kabla ya kuwasili kwa bidhaa.
Nyaraka za kuingiza bidhaa zinajumuisha.
- Ankara ya Mwisho
- Barua ya Kumwidhinisha Wakala kutoka kwa mwingizaji mzigo
- Vibali vya kuingiza bidhaa kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA, Shirika la Viwango Tanzania(TBS)
- Nyaraka za msamaha wa kodi (Kama zipo)
- Orodha ya Ufungashaji
- Nyaraka za usafirishaji, yaani Hati ya Kupokea Mzigo Bandarini/Hati ya Kupokea Mzigo Uwanja wa Ndege/Taarifa za mzigo uliosafirishwa kwa njia ya barabara.
- Taarifa kuhusu Fedha Taslimu na Hati za Malipo zinazosafirishwa kuingia au kutoka nje ya Nchi
Angalizo;
Mfumo wa uondoshaji mizigo (TANCIS) utakataa kupokea tamko ambalo halijakamilika kielekitroniki au lenye maelezo pungufu kupitia katika mfumo wake wa maulizo (IQS).
Habari & Matukio
Ufanisi wa Bandari umeongeza mapato ya Serikali
Mwenyekiti wa Bodi aonyesha njia TRA kuvuka malengo