Utaratibu wa kuomba Leseni za Forodha
Mtu yeyote anayetaka kuondosha mizigo/bidhaa kwenye maeneo ya forodha kwa niaba ya waingizaji bidhaa na mtu yeyote anayetaka kufanya biashara yeyote kati ya biashara zifuatazo,Maghala ya dhamana ya Forodha,Uzalishaji bidhaa chini ya utaratibu wa ghala za dhamana za forodha,Usafirishaji wa bidhaa zilizopo chini ya udhibiti wa forodha,Bandari kavu na ya vituo vya usafirishaji wa makasha wanakaribishwa kuwasilisha maombi ya leseni ya kuendesha biashara hiyo kwa Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa ili mradi wanakidhi masharti ya leseni husika ya kundi linalohusiana na leseni wanayoomba.
A) MASHARTI YA JUMLA (Kwa ajili ya Makundi ya leseni zote)
Waombaji wote wanatakiwa kuwa na nyaraka na viambatishi vilivyoorodheshwa hapa chini:
- Cheti cha Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi cha Kampuni (TIN)(Kwa waombaji wapya)
- Cheti cha usajili wa Kampuni (kwa Waombaji wapya tu)
- Cheti cha Utambulisho wa Mlipakodi kwa kila Murugenzi (kwa Waombaji wapya tu)
- Cheti cha usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani, kama kipo,
- Hati ya malipo ya kodi kilichotolewa hivi karibuni.
- Malengo na Katiba ya Kampuni (Kwa Waombaji wapya)
- Nakala iliyoidhinishwa ya cheti cha Usajili wa Kampuni na cheti cha usajili wa jina la Biashara, vinapohitajika (kwa waombaji wapya)
- Picha ya pasipoti ya hivi karibuni (isizidi megabiti moja) ya Wakurugenzi na watumishi zilizoidhinishwa na Kamishna wa Viapo au Wakili (kwa waombaji wapya na wale wanaohuisha kama kuna mabadiliko)
- Nyaraka hai za utambulisho kwa kila mhusika kwenye kipengere cha (7) hapo juu ambavyo ni Kitambulisho cha Taifa, Hati ya kusafiri, Kitambulisho cha Mpiga kura kwa Waombaji wapya na wanaohuisha tu ikiwa kuna mabadiliko)
- Barua kutoka kwa mdhamini/Wadhamini inayothibitisha kuwa Bima au dhamana husika italipa endapo kutakuwa na upotevu wa kodi za Serikali (kwa wanaohuisha),au dhamana husika za forodha (kwa ajili ya Waombaji kabla ya leseni haijatolewa).
- Nakala iliyoidhinishwa ya hati ya nyumba au mkataba wa pango kwa ajili ya ofisi ya kampuni. Ofisi hiyo inatakiwa kuwa na vitendea kazi vya kompyuta vitakavyounganishwa na mfumo wa pamoja wa forodha Tanzania(TANCIS)-vitakavyothibitishwa kaba leseni haijatolewa
- Kusiwepo na madai yoyote yanayohusiana na ushuru wa forodha kama vile hoja ya ukaguzi,TANSAD ambayo haijalipwa,madai ya miamala ya mizigo inayopita hapa nchini kwenda nchi za nje au suala lolote la ushuru wa forodha ambalo halijatatuliwa (kwa wanaohuisha).
- Barua toka Wakala wa Usajili wa Makampuni na Biashsara na Leseni inayoelezea hali ya sasa ya Wakurugenzi wa Kampuni na Wanahisa (kwa waombaji wapya and wanaohuisha tu kama kuna mabadiliko)
B) Masharti maalumu (Kwa Mawakala wa Forodha)
Maombi mapya na kwa wale wanaohuisha leseni yatapokelewa na kuchakatwa kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa pamoja wa Forodha(TANCIS). Waombaji wapya wa leseni za Uwakala wa Forodha wanatakiwa kuzingatia yafuatayo;
a) Kuchukua nywila ya Kampuni ambayo itahitajika wakati wa kuchakata maombi.
FOMU ZA MAOMBI YA NYWILA namba F-ITD-067 inapatikana kwenye tovuti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (www.tra.go.tz).fomu.
Utaratibu wa mafunzo kwa WAOMBAJI WAPYA UTAENDESHWA KAMA UTAKAVYOELEKEZWA KWENYE TANGAZO.
b) Pakua fomu ya maombi ya Uwakala wa Leseni (C.20) inayopatikana katika Tovuti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (www.tr.go.tz).fomu. Maombi yanatakiwa kujazwa kwa ukamilifu na kusainiwa na Mkurugenzi wa Kampuni na kuambatanishwa na nyaraka zilizothibitishwa ambazo zimeorodheshwa katika kipengere A (Masharti ya jumla kwa ajili ya makundi yote ya leseni).
c) Malipo ya ada kasi cha Dola za Kimarekani 50,ambayo hayarudishwi
d) Kuwa na angalau waajiriwa wawili Mkuu wa Uondoshaji bidhaa bandarini mwenye elimu ngazi ya Astashahada,cheti kutoka chuo kinacho tambulika au mwenye uzoefu usiopungua miaka mitano katika shughuli za Forodha.
e) Kuwasilisha barua ya utambulisho nakala mbili ambazo zitakuwa zimebandikwa picha za pasipoti ya mtumishi mmojawapo mwenye uelewa atakayewakilisha Kampuni kwenye usaili barua hiyo inatakiwa iwe na barua pepe na namba ya simu na kuelezea ya kwamba Bwana/Bi amekidhi masharti yafuatayo;
i) Bwana/Bi ni Mkurugenzi au Mtumishi wa Kudumu wa Kampuni
ii) Mwenye cheti cha Forodha cha Afrika Masahariki ya kufanya kazi za kupokea na kuondosha bidhaa
iii) Hajawahi kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ambayo leseni yake ya uwakala wa Forodha imewahi kufutwa.
iv) Mtahiniwa aliyefanya usaili na kufaulu kwa ajili ya kampuni, hataruhusiwa kufanya usaili kwa Kampuni nyingine.
f) Kuwasilisha kiapo kilichosainiwa na Kamishna wa Kiapo pamoja na maelezo yafuatayo;
i) Hajawahi kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ambayo leseni yake imefutwa ndani ya miaka mitano iliyopita.
ii) Sio Mkurugenzi wa Kampuni wa Kampuni ambayo leseni yake iko hai.
iii) Mkurugenzi au Mwanahisa wa Kampuni sio mwajiriwa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
iv) Kampuni itatoa huduma za msingi za Forodha kwa saa 24 kwa siku 7.
v) Kampuni ambayo haijihusishi au haina udhibiti na shughuli za Kampuni ambayo inayofanya na kuhifadhi bidhaa zinazoingia nchini baada ya kushushwa kutoka kwenye meli au ndege na bidhaa zinazosafirishwa nje ya nchi zilizopakiwa kwenye meli au ndege.
g) Waombaji wapya wataingia kwenye dhamana ya forodha ya kiasi cha shilingi za Kitanzania Milioni Mia Moja (100,000,000/=) na kuwasilisha baada ya kufaulu mtihani.
2. Maombi ya kuhuisha leseni ya Uwakala wa Forodha yanapokelewa na kuchakatwa kupitia mfumo wa pamoja wa forodha(TANCIS) na inatakiwa kuambatana na;
a) Ada ya maombi isiyorudishwa ya dola za Kimarekani 50.
b) Cheti cha usajili wa Uwakala wa forodha kinachotolewa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC).
c) Uthibitisho wa Ushiriki au uanachama kwenye chama cha wapokeaji na wasafirishaji wa mizigo kinachotambulika kwa mfano TAFFA.
d) Leseni ya forodha iliyo hai kwa mwaka unaofuata.
Angalizo: Orodha ya waombaji wa leseni ya uwakala wa forodha watakaochaguliwa ndio watakaojulishwa kupitia mfumo wa pamoja wa forodha Tanzania(TANCIS).
C)MASHARTI MAALUMU (Kwa ajili ya Maghala ya Dhamana ya Forodha(CBW) na Waendeshaji wa Uzalishaji chini ya Dhamana(MUB).
1.Maombi ya leseni kwa ajili ya kuendesha Maghala ya Dhamana ya Forodha na Uzalishaji chini ya Dhamana ya forodha amabao yanakidhi masharti ya jumla kama ilivyoainishwa katika kipengere (A) hapo juu na kutakiwa kuzingatia yafuatayo;
(a) Pakua fomu ya maombi ya forodha (C.18) inayopatikana kwenye tovuti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania(www.tra.go.tz) Waombaji wanatakiwa kujaza fomu ya maombi na inatakiwa isainiwe na Mkurugenzi wa Kampuni ikiambatana na nyaraka zilizothibitishwa na kuorodheshwa chini ya kipengere A (Masharti ya jumla ya leseni kwa ajili ya makundi yote)
(b)Kuwasilisha mchoro uliochorwa kitaalamu wa majengo ya eneo husika ikihusisha majengo yanayozuguka eneo hilo na jinsi mazingira ya eneo zima yanavyoonekana kwa uwazi.
(c)Kukidhi kiwango cha chini katika eneo ambalo lenye mita za mraba 1000 na 2000 kwa ajili ya Maghala ya Dhamana ya Forodha ya binafsi na Maghala ya Dhamana ya Forodha ya Jumla kwa mfuatano;
(d)Jengo linatakiwa liwe katika eneo la viwanda au biashara.
(e)Kuwasilisha nakala iliyoidhinishwa ya mkataba wa pango ambao kipindi chake ni kirefu kuliko kipindi cha leseni iliyoombwa au kuleta uthibitisho wa umilki wa jengo.
(f) Iwe na eneo la kutosha la maegesho au eneo la kuhifadhi lilotengenezwa kwa matofali madogo ya sementi, lami au zege imar
(g) Jengo linatakiwa liwe na usalama na ambalo lina uzio wenye urefu wa mita tatu, na ukuta wa zege na waya zenye umeme na mwanga.
(h) Jengo linatakiwa liwe na usalama na ulinzi saa 24 ikiwa ni pamoja na ulinzi wa kamera.
(i) Jengo liwe na vifaa vya kuzima moto.
(j) Kuwasilisha fomula ya uzalishaji iliyoidhinishwa na Shirika la Viwango Tanzania na Mamlak nyingine kwa uzalishaji chini ya Dhamana(MUB)
(k) Kuwasilisha leseni ya viwanda iliyotolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara (Kwa ajili ya wazalishaji chini ya dhamana).
Baada ya kukamilisha hayo hapo juu, unatakiwa kuweka dhamana kwa kutumia fomu ya forodha ya dhamana na mdhamini aliyesajiliwa mwenye leseni kama ifuatavyo;
Ghala Binafsi la -kiasi kisichopungua shilingi 500,000,000/=
Ghala la Dhamana la Kawaida-kiasi kisichopungua shilingi1,000,000,000/=
Ghala la Dhamana la uzalishaji chini ya Dhamana-kiasi kisichopungua shilingi 2,000,000,000/=
Kwa nyongeza ya hapo juu ya dhamana, waombaji waliokubaliwa wanatakiwa kuweka dhamana ya forodha ili kulinda uondoshaji wa mizigo kutoka na kwenda katika maghala ya forodha ya dhamana/maghala ya dhamana chini uzalishaji kwa kiwango kisichopungua shilingi 100,000,000/=.
2.Maombi ya kuhuisha leseni ya kuendesha Maghala ya Dhamana ya Forodha na Maghala ya uzalishaji chini ya dhamana yanaombwa kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa pamoja wa Forodha Tanzania.
C) MASHARTI MAALUMU (Kwa ajili ya Wasafirishaji wa Bidhaa chini ya Udhibiti wa Forodha)
Waombaji wote wa leseni za usafirishaji na leseni za magari wanatakiwa kuzingatia masharti ya nyongeza yafuatayo;
1.Kuweka dhamana ya forodha kiasi cha shilingi za Kitanzania (10,000,000/=, kwa C. 28 au C. 40) au milioni Hamsini (50,000,000/=) kwa leseni zote mbili (C. 28 na C. 40).
2.Kuwasilisha leseni ya gari ya uchukuzi inayotolewa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)
3.Kuwasilisha barua ya kuhuisha dhamana yenye kudhibitisha marejesho ya kila mwaka kwa dhamana ya kiasi cha shilingi za Kitanzania 10,000,000/= au 50,000,000/= kutoka kwa mdhamini ukiambatashanisha nakala halisi ya dhamana ambayo inatakiwa kuhuishwa. (Kwa wale wanaohuisha).
4.Mhusika anayehusika moja kwa moja kushughulikia nyaraka za forodha au kushughulika na forodha lazima wawe Wakurugenzi/Wamiliki/Waajiriwa kama ilivyoanishwa kwenye masharti ya jumla katika sehemu A.
5.Uthibitisho wa ushiriki au uanachama kwenye chama kinacho tambulika.
6.Omba cheti cha kuwa Msafirishaji.
7.Kila mtu anayefanya shughuli hii ni lazima awe na leseni kwa kutumia fomu C. 28 na C. 40 inayolipiwa ada ya Dola za Kimarekani (200) kwa mfuatano kulingana na Kanuni ya Usimamizi ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya 2010.
E ) MASHARTI MAALUMU KWA AJILI YA BANDARI YA NCHI KAVU NA VITUO KUJAZA MAKASHA KWA AJILI YA KUSAFIRISHA NJE YA NCHI
Maombi ya Bandari Kavu na Vituo vya kujazia makasha kwa ajili ya kusafirisha makasha yanafanyika kwa kutumia fomu (fomu C. 18) na ni lazima yafanyike kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa pamoja wa forodha na waombaji wanatakiwa kuzingatia masharti yafuatayo;
1.Mahali: Bandari Kavu ni lazima iwe kilomita 30 au zaidi kutoka bandarini. (kwa waombaji wapya).
2.Uzio: Ukuta imara wa zege angalau uwe na urefu wa mita 3 kwenda juu, uliozungushwa na waya wenye umeme
3.Milango ya Kuingia /Kutoka: Inatakiwa iwepo milango miwili tofauti wa kuingilia na kutoka.
4.Ulinzi: Ulinzi saa 24 ikiwemo ulinzi wa askari na kamera.
5.Eneo la Maegesho: Bandari ya nchi kavu na vituo vya kujazia na kusafirisha makasha ni eneo la forodha ambalo linaweza huruhusu magari kupakia na kupakua. Kwa hiyo eneo la maegesho lazima liwe nje ya mipaka ya bandari ya nchi kavu na vituo vya usafirishaji kwa ajili ya magari yanayosubiri, wakati wa kupakia.
6.Kusakafia/kuweka zege: Kwa madhumuni ya uimarishaji na madhubuti, sakafu ya eneo inatakiwa iwe ya zege, iwe imara kuhimili uzito wa magari mazito na iwekwe miundombinu ya kutolea maji.
7.Mpaka: kuwepo na mpaka wa kutenganisha sehemu ya bidhaa zinazingia nchini na zinazosafirishwa nje ya nchi kwa bidhaa zilizo hakikiwa na iwepo sehemu ya makasha matupu.
8.Eneo la Ukaguzi: Eneo hili linatakiwa liwe limepigwa bati na lenye eneo la kukagulia lenye ukubwa wa kukagulia makontena 10 ya futi 20 kwa wakati mmoja.
9.Kibanda cha mizigo inayosafirishwa nje ya nchi: Ni mahsusi kwa bbidhaa ambazo haziwezi kutosha tena kwenye makasha baada ya kupakuliwa wakati wa ukaguzi, kibanda hichi kinatakiwa kiwe na ukubwa unatosheleza.
10.Ghala la Forodha: Ukubwa wa ghala la forodha linatakiwa liwe na angalau mita za mraba 300.
11.Ofisi ya Forodha: Inatakiwa iwe na uwezo wa kukaliwa na angalau maofisa 5 wa forodha na iwe na samani, hewa ya kutosha, mwanga, simu, usafi na vitu vingine vya lazima.
12.Vifaa: Panatakiwa pawe na vifaa kwa ajili ya kushughulikia bidhaa, kupanga, kupima wakati wa ukaguzi. Kwa kuongezea inatakiwa kuwe na angalau mitambo viwili ya kupangia bidhaa kwa ajili ya urahisishaji mtambo mmoja unapopata hitilafu. 13.Dhamana: Baada ya kukamilisha masharti ya hapo juu na kabla ya leseni kutolewa, waombaj ni lazima kuweka dhamana ya forodha kama ifuatavyo;
CB 2 angalau shilingi za Kitanzania 500,000,000/=
CB 13 Angalau shilingi za Kitanzania 2,000,000,000/=
14.Wafanyakazi: Bandari ya nchi kavu na vituo vya kusafirisha makasha wanatakiwa wawe na wafanyakazi wanaotosha wakati wote.
15. Ukubwa wa Bandari ya Nchi kavu na Vituo vya kujazia makasha yanatakiwa yawe na ukubwa wa angalau mita za mraba 40,000 kwa Bandari ya Nchi Kavu na mita za mraba 10,000 kwa Vituo vya kujazia makasha kwa ajili ya Kusafirisha.
16. Muunganiko na reli : Bandari kavu na Vituo vya kusafirishia makasha vinatakiwa view na muunganiko na reli.
17. Pango la Ardhi: Bandari ya nchi kavu na vituo vya kujazia na kusafirishia makasha vinatakiwa aidha viwe na hati milki au mkataba wa pango kwa ajili ya ardhi ambayo Bandari ya nchi kavuna vituo vya kujazia na kusafirishia makasha ambayo ni hai hadi kufikia kabla ya mwezi Juni ya mwaka wa maombi.
18. Muda wa kazi: Waombaji waliopata leseni wanatakiwa kuwa na utaratibu wa kufanya kazi kwa muda wa saa 24 kwa siku 7.
19. Mwanga: Taa za mwanga mkali zinatakiwa ziwekwe na kuwaka katika eneo husika kuweza kusaidia kazi zifanyike kwa saa zote 24 .
20. Mamlaka ya Wakala wa Meli: Kuwasilisha leseni kwa ajili ya Bandari ya nchi kavu na Vituo vya kujazia na Kusafirishia Makasha (Kwa waombaji wapya na wanaohuisha).
21. Wakala wa Barabara Tanzania: Kuwasilisha barua ya kuruhusu kutoka Wakala wa Barabara (kwa wote wawili, waombaji wapya na wanahuisha).
Kwa mujibu wa sharia ya Forodha ya Afrika Mashariki yam waka 2004 Leseni zote zinatakiwa ziwe halali kwa mwaka wa kalenda ambao unaanza tarehe 01 Januari hadi Disemba ya kila mwaka.
Habari & Matukio
Ufanisi wa Bandari umeongeza mapato ya Serikali
Mwenyekiti wa Bodi aonyesha njia TRA kuvuka malengo