Emblem TRA Logo
Usajili wa Vyombo vya Usafiri

Utangulizi:

Vyombo vya usafiri vinatumiwa na watu wengi na wasiobainishwa katika barabara za umma na wanatambuliwa kijamii mara baada ya kukaguliwa na kusajiliwa. Vyombo vya usafiri pia vinaharibika na kuchakaa kimuundo na vifaa na wakati mwingine maumbo yao na kurekebishwa.

Ni sheria zipi zinasimamia usajili wa vyombo vya usafiri?

Usajili wa vyombo vya usafiri Tanzania bara unasimamiwa na:

  • Sheria Na. 30 ya usalama barabarani ya mwaka 1973
  • Sheria ya Vyombo vya usafiri (Kodi ya usajili na ubadilisha wa umiliki) ya mwaka 1972
  • Kanuni za usalama barabarani (magari ya kutoka nje ya nchi) ya mwaka 1973
  • Taratibu za usalama barabarani (usajili wa vyombo vya usafiri) (marekebisho) ya mwaka 2001

Taratibu za usajili

Usajili wa umiliki wa chombo cha moto unamtaka mtu awe na miaka 18 na zaidi ili aweze kusajiliwa kama mmiliki wa chombo cha moto, na miaka 14 na zaidi ili kusajiiwa kama mmiliki wa pikipiki. Zaidi ya hayo usajili unafanyika kwa watu wenye akili timamu tu.

Utaratibu wa Usajili Vyombo vya Moto

Nyaraka zifuatazo zinapaswa kuwasilishwa kwenye ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania:

  • Fomu ya maombi ya usajili wa vyombo vya moto (MV 10) iliyojazwa kwa usahihi na mwombaji
  • Tamko la forodha: Waraka Mmoja wa Usimamizi Tanzania na kibali cha kuruhusu kutoa mzigo
  • Hati ya malipo ya benki kuthibitisha ushuru uliolipwa.
  • Nakala ya hati yako ya namba ya utambulisho wa mlipa kodi
  • Hati ya kufuta usajili au kadi ya usajili (magari yaliyotumika)
  • Barua ya polisi wa kimataifa (kama gari limeingizwa kutoka kwenye nchi mwanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika
  • Ankara ya kodi (kama gari limenunuliwa kwa muuza magari wa ndani)

Maombi ya usajili wa vyombo vya usafiri

Kila mtu anayemiliki chombo cha usafiri atapaswa kutoa maombi kwa kujaza fomu MV 10 kwa ajili ya usajili wa chombo husika, isipokuwa katika yafuatayo:

  • vyombo vya usafiri vinavyomilikiwa na serikali,
  • Jeshi la Wananchi wa Tanzania,
  • Mashirika ya kimataifa
  • Ofisi za kidiplomasia au balozi ndogo

Kadi zilizopotea za usajili wa vyombo vya usafiri

Utaratibu wa kufuata pindi mmiliki wa vyombo vya moto anapopotelewa na Kadi.

1. Kutoa tangazo kwenye gazeti kuhusu kupotelewa na kadi ya gari akitaja namba ya gari na mahali ilipopotelea.

2. Atume barua kwa Meneja wa Mapato Mkoa akiomba kupatiwa nakala ya kadi.

3. Atatakiwa kujaza Fomu ya maombi – MV 40, akiambatanisha na: -

(i) Nakala ya tangazo alilotoa katika gazeti

(ii) Taarifa ya Polisi kuhusu kupotea kwa Kadi ya usajili wa gari

(iii) Taarifa ya ukaguzi wa gari toka Polisi

(iv) Nakala halisi ya kitambulisho kimojawapo (Leseni ya udereva, Kitambulisho cha Taifa, hati ya kusafiria au Kadi ya mpiga kura. Aidha, atatakiwa kuleta nakala moja ambayo itakuwa imegongwa muhuri na Wakili aliyesajiliwa Kisheria/Hakimu.

(v) Kiapo cha Mahakama kuhusu umiliki wa gari na kutaja namba ya gari lake.

(vi) Gari itatakiwa kuletwa katika ofisi za TRA kwa ajili ya kukaguliwa na Afisa wa TRA.

(vii) Picha ya Mmiliki wa gari Pasipoti size iliyopigwa siku za karibuni.

(viii) Namba ya simu anayotumia na ambayo itahakikiwa kuwa ni ya kwake.

(ix) Kivuli cha Kadi ya gari iliyopotea

(x) Endapo TRA haitapokea pingamizi lolote Baada ya siku 30 tangu kutolewa tangazo kwenye gazeti juu ya kupotelewa Kadi ya gari mhusika atajulishwa na atatakiwa kulipia Ada ya shilingi 70,000 na kupatiwa nakala ya Kadi husika.

Ada za usajili wa vyombo vya usafiri

Ada ya usajili wa chombo cha Moto kwa mara ya kwanza pamoja na ada za leseni ya chombo cha moto yanayotumia nishati aina zote

 

Kodi ya Usajili Kuhusuana na Magari     ADA
Magari yenye uwezo wowote wa silindaTshs. 250,000/=
Magari mengineTshs   250,000/=
Nambari Binafsi ya chombo cha motoTshs. 5,000,000/= kwa miaka 3
Nambari Maalum ya Usajili pamoja na ada ya usajiliTshs. 500,000/=
  
Kodi ya Usajili kwa Gari la Umeme au Gari la Mseto la Umeme
Mseto mdogo wenye uwezo wa 5< KwTshs. 95,000/=
Mseto mdogo au nusu-mseto na uwezo wa 6-30 Kw,      Mseto kamili wenye uwezo wa Kw 31-40, mseto wa programu-jalizi wenye uwezo wa Kw 41-90             Tshs. 250,000/=
Pikipiki iwe ya umeme au vinginevyoTsh. 95,000/=
  
Ada ya Usajili wa Leseni ya Magari kwenye Usajili wa Kwanza hutegemea uwezo wa Injini ya Gari.

501 – 1500 cc

Tshs 200,000/=

1501 – 2500cc

Tshs. 250,000/=

2501 na kuendelea

Tshs. 300,000/=
Pikipiki au Bajaji ya Matairi matatu inayojulikana kama Bajaji, iwe ya umeme au laTshs.    50,000/=
Ada ya leseni ya gari inayotozwa wakati wa kutoa cheti cha usajili kwenye gari la kuchaji Umeme
Micro Hybrid yenye uwezo wa 5< KwTshs. 50,000.00
Mseto mdogo/nusu wenye uwezo wa Kw 6-30Tshs. 200,000.00
Mseto Kamili wenye uwezo wa 31-40 KwTshs. 250,000.00
Plug Hybrid yenye uwezo wa 41-90 Kw Tshs. 300,000.00

Watengenezaji wa vibao vya namba za vyombo vya usafiri

 

Mkurugenzi Mtendaji

Masasi signs company Limited

S.L.P 12848

Dar es salaam

22118260

Mkurugenzi Mtendaji

Autozone Limited

S.L.P 6560

Dar es salaam

0655/782752837

Mkurugenzi Mtendaji

Signs Industries Limited

S.L.P 1965

Dar es salaam

2866500/2860440

Mkurugenzi Mtendaji

Budda Auto Parts

S.L.P 4763

Mkunazini

Zanzibar

2231707/0777411149

Mkurugenzi Mtendaji

Parkison Clarke Plate Maker Ltd

S.L.P 4298

Dar es salaam

+255683466080

Mkurugenzi Mtendaji

Kiboko Pre-coated Sheets Limited

S.L.P 3030

Dar es salaam

+255683522100/+255787970645

Mkurugenzi Mtendaji

Next Telecom Int (T) Ltd and Erich Utsch AG

S.L.P 8173

Dar es salaam

0773290500 

Mkurugenzi Mtendaji

Muki (T) Limited

P.O. Box 7261

Dar es Salaam

Samora-Puma Building

0715001542/0712221882/

0622564442