Tarehe Zipi ni Muafaka Kulipa Ushuru na Kodi?
Kodi ya Mapato
Kodi zinazolipwa kwa awamu (kodi zinazokadiriwa kwa awamu) zinazilipwa katika kila robo mwaka; kwa mfano walipakodi ambao vipindi vyao vya kulipa vinaisha tarehe 30 Desemba; awamu za malipo zitafikia wakati wa kulipwa mwishoni mwa Machi, Juni, Septemba na Desemba.
Kodi za zuio zinalipwa ndani ya siku 7 baada ya mwisho wa mwezi wa kalenda ambayo kodi hiyo inahusika.
Kodi itokanayo na pato la ajira (PAYE) inalipwa ndani ya siku saba (7) baada ya kuisha mwezi wa kodi husika.
Kodi ya Kujikadiria Dharura inalipwa katika tarehe iliyobainishwa katika taarifa ya makadirio.
Kodi Iliyorekebishwa inalipwa ndani ya siku 30 tangu tarehe ya makadirio.
Kodi ya kidigitali inalipwa ndani ya siku 20 baada ya kuisha mwezi wa kodi husika.
Kodi ya halisi ya mwisho italipwa tarehe ya mwisho ya ritani ya mapato (miezi sita baada ya mwaka wa mapato).
SDL
Kodi ya maendeleo ya ujuzi (SDL) inalipwa ndani ya siku saba (7) baada ya kuisha mwezi wa kodi husika.
Ushuru wa Bidhaa
Ushuru wa Bidhaa inalipwa ndani ya siku ishirini na tano (25) baada ya kuisha mwezi wa kodi husika.
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
VAT inadaiwa na inalipwa kabla au kabla ya siku ya 20 ya mwezi unaofuata mwezi wa biashara ambayo mapato yanahusiana. Mlipakodi anahitajika kuwasilisha marejesho ikiwa mtu huyo ana kiasi halisi cha kodi ya ongezeko la thamani inayolipwa kwa kipindi hicho.
Kuongeza Muda wa Kulipa Kodi
Mlipakodi anaweza kuomba kwa maandishi kwa kamishna mkuu kuongezewa muda wa kulipa kodi kwa mujibu wa sheria.Kamishna mkuu kufuatia kupokea maombi hayo yakionyesha sababu ya msingi anaweza kusogeza tarehe ya kulipwa kodi au sehemu ya kodi.
Kamishna mkuu atamjulisha mwombaji kwa maandishi, maamuzi juu ya maombi yake.Na pale ambapo kibali kimetolewa kwa kumruhusu mlipakodi kulipa kodi kwa awamu na mlipakodi ameshindwa kulipa awamu yoyote,kiasi chote cha deni la kodi jumlisha riba italipwa mara moja.
Habari & Matukio