Tamko Kabla ya Mzigo Kufika ni Nini?
Tamko Kabla ya Mzigo Kufika ni nyenzo katika mfumo wa kuondosha mizigo ambao unaruhusu Mwingizaji wa Mzigo/Wakala kuanza taratibu za kuondosha mzigo kabla ya kuwasili kwa bidhaa sehemu bidhaa zinapoingilia.nyenzo hii inawasaidia Waingizaji wa mzigo kukamilisha taratibu kabla ya kuwasili kwa bidhaa kwa sababu ya kupunguza muda utakaotumika katika kuondosha bidhaa punde bidhaa zitakapowasili. Hata hivyo, mchakato wa awali unaanza na mwingizaji wa mzigo kupitia Wakala wake wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo aliyeteuliwa.
Angalizo: Nyenzo hii inatumika katika bidhaa zote zinazo ingizwa nchini isipokuwa kwenye uingizaji wa mafuta(Mazao Meupe),bidhaa zinazoingia vya vifurushi kupitia Posta na huduma ya vifurushi,bidhaa zinazoingia kwa muda ,bidhaa zinazoondoshwa chini ya matamko ya awali na matamko ya mizigo inayopitishwa kwenda nchi nyingine.
Uhakiki wa Bidhaa
Bidhaa zinazoingia zinatakiwa zifanyiwe uchaguzi utakaobainisha kama bidhaa zinatakiwa ziondolewe moja kwa moja (KIJANI) zifanyiwe ukaguzi wa nyaraka (NJANO), kupiga picha au ukaguzi wa bidhaa (NYEKUNDU). Ubainishaji wa uchaguliwaji unafanyika na mfumo kupitia usimamizi wa hatari ambapo kigezo ikijumuisha asili ya bidhaa,mwingizaji, Wakala na aina ya bidhaa, bidhaa zinakaguliwa na kuondolewa kutoka bandari, vituo vya mipaka au kiwanja cha ndege.
MFUMO WA PAMOJA WA FORODHA
- Mwingizaji bidhaa nchini kupitia kwa wakala atapakia nyaraka kwenye mfumo kwa njia ya kieletroniki akiambatanisha na nyaraka zinazohitajika.
- Ikiwa tamko litakataliwa Wakala wa kupokea na kusafirisha bidhaa anatakiwa kuwasilisha tamko jipya kulingalinalozingatia mahitajai ya mfumo wa Pamoja wa Forodha Tanzania.
- Kadhia moja ya Forodha Tanzania itachakatwa hadi katika hatua ya malipo kabla orodha ya shehena haijawasilishwa.
- Orodha ya shehena inahamishwa kwenda kwenye hatua ya kuruhusu hati ya forodha ya kutolea mzigo.
- Wakala wa kupokea na kusafirisha mizigo atapata Taarifa ya Kukubaliwa pamoja na Taarifa ya malipo iliyoandaliwa kwa kuzingatia Thamani iliyotamkwa.
- Wakala wa kupokea na kusafirisha Mizigo atapata taarifa ya marekebisho mara marekebisho yanapokuwa yamepitia ukaguzi na kumalizika.iwapo afisa amebatilisha marekebisho Wakala wa kupokea na kusafirisha Mizigo atapata taarifa ya kukataliwa kwa marekebisho ya kadhia moja ya forodha Tanzania,vinginevyo afisa atairudia kuishughulikia katika uainishaji wa nyaraka,kuthaminisha na kuhakiki
- Mara uhakiki unapokuwa umekamilika, matokeo yatasajiliwa na afisa husika.
- Matokeo ya uhakiki yatawasilishwa kwa msimamizi kwa ajili ya kuidhinishwa.Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo atapokea Taarifa za Makadirio.
- Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo anapaswa kukubali au kupinga Taarifa ya Makadirio
- Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo anapaswa kupinga Makadirio ya Afisa kupitia Mfumo wa Pamoja wa Maulizo
- Iwapo Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo anakubali Taarifa na makadirio yameongozeka ikilinganishwa na thamani iliyotajwa, Taarifa ya Malipo ya Ziada itatolewa ndani ya taarifa ya makadirio. Taarifa hii ya thamani ya malipo itakuwa tofauti ya kiasi cha mwisho na taarifa ya malipo iliyotolewa awali.
- Iwapo kutakuwa na tofauti kati ya data ya orodha ya shehena na tamko, Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo atapokea Taarifa ya Kunyimwa Kibali. Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo atapaswa kurekebisha tamko kama atakavyoelekezwa na matokeo ya ukaguzi na kuliwasilisha tena.
- Malipo yatakapokuwa yamepokelewa, ukaguzi kukamilika ipasavyo, Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo atapokea Kibali cha Kutoa Mzigo husika.
Mchakato huu unachukua muda gani kabla ya kupata mizigo?
Jumla ya saa 24 (siku 1) zimepangwa kwa ajili ya kushughulikia Tamko Kabla ya Kuwasili kwa Mzigo kuanzia usajili hadi utoaji wa ripoti muhimu za kutoa mzigo (Makadirio Halisi ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika) kwa Tamko Kabla ya Kuwasili kwa Mzigo zilizowasilishwa pamoja na au baada ya kupokea nyaraka za kutosha ambazo zinakidhi viwango vinavyotakiwa.
Makadirio ya Awali ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika kwa Taarifa Kabla ya Kuwasili kwa Mzigo zilizowasilishwa pamoja na seti kamili ya nyaraka za mwisho zinapaswa kushughulikiwa na kutolewa ndani ya saa 24.
Angalizo: Makadirio ya Awali ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika kwa Taarifa Kabla ya Kuwasili kwa Mzigo zilizosajiliwa bila seti kamili ya nyaraka za mwisho zinapaswa kushughulikiwa na kutolewa saa 24 baada ya kupokea Taarifa Kabla ya Kuwasili kwa Mzigo, yaani iwapo nyaraka za mwisho zinapokelewa baada ya wiki mbili, mchakato unaanzia siku hiyo.
Makadirio Halisi ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika yanapaswa kushughulikiwa na kutolewa ndani ya saa 24 baada ya kupokea maombi ya Makadirio Halisi ya Tamko Kabla ya Mzigo Kufika pamoja na seti kamili ya nyaraka zinazohitajika.
Baada ya kujaza Waraka Mmoja Wa Usimamizi Tanzania na malipo ya ushuru kama upo, uchaguzi utafanyika ndani ya saa 24.
Mizigo inateuliwa kwa itakayoruhusiwa kutolewa moja kwa moja, ya kijani itapata kibali cha kutolewa bandarini au mahali pa kuingizia mizigo, ile iliyochaguliwa kwa ajili ya ukaguzi wa nyaraka itakaguliwa katika Kituo cha Huduma cha Forodha(CSC), na ile iliyochaguliwa kwa ajili ya ukaguzi wa kiupekuzi na kuruhusiwa kutolewa bandarini na mahali pa kuingilia.
Angalizo: Mfumo wa Pamoja wa Forodha Tanzania unatumika Vituo vyote vya Forodha Tanzania Bara na Zanzibar.
Habari & Matukio
Ufanisi wa Bandari umeongeza mapato ya Serikali
Mwenyekiti wa Bodi aonyesha njia TRA kuvuka malengo