Utangulizi
Sheria ya Ushuru wa Stempu, 1972 ilianza kutumika mnamo mwezi Julai 1, 1972. Ilitangua Sheria ya Stempu. Malengo yake yaliwekwa kuunganisha na kurekebisha sheria inayohusiana na ushuru wa stempu, kwa kuweka marekebisho madogo, mengi yao yalikuwa ya kiutaratibu. Masharti yanayohusiana na mikataba ya pamoja yalifafanuliwa. Masharti maalum yanayohusiana na makosa yaliingizwa.
Nyaraka zipi zinahusishwa na Ushuru wa Stempu?
Nyaraka za kisheria zilizofafanuliwa kwenye jedwali ambazo zilizotumika Tanganyika (Tanzania bara) au kama zilivyotumika nje ya Tanganyika zinazohusiana na mali yoyote au masuala yoyote au jambo lililofanyika Tanganyika, lazima zitozwe ushuru kiasi ambacho kimetajwa au kukokotolewa kwa namna ilivyoelezwa kwenye jedwali kuhusiana na sheria hiyo isipokuwa kama zina msamaha wa Ushuru wa Stamp.
Sheria ya Ushuru wa Stempu inabainisha watu watakaolipa ushuru wa stempu ambapo mara nyingi hulipwa na mtu anayeandika, kuandaa au kutumia waraka wa kisheria. Iwapo mtu anakuwa na mashaka kama iwapo waraka wa kisheria unapaswa au haupaswi kubandikwa stempu au kuhusu kiasi cha Ushuru wa Stempu kinacholipwa kuhusiana na waraka wowote wa kisheria, anaweza kupeleka suala hilo kwa Afisa Ushuru wa Stempu kwa ajili ya uamuzi.
Usimamizi wa Ushuru wa Stempu
Wakati ambapo Hati Zinapaswa Kubandikwa Stempu
Hati zote zinazotozwa ushuru wa stempu zinazotumiwa na mtu yeyote Tanzania Bara zinapaswa kubandikwa stempu ndani ya siku thelathini za kutumika:
Iwapo hati imeletwa kwa afisa husika kwa ajili ya uamuzi, inapaswa kubandikwa stempu ndani ya siku thelethini, tangu wakati wa uwasilishaji wa hati hiyo kwa afisa husika hadi wakati taarifa itakapomfikia mtu aliyeiwasilisha kuhusu uamuzi wa afisa husika, siku hizo zitaondolewa katika kukokotoa siku hizo thelathini; na kila risiti, kukiri kuhusu deni, taarifa ya ahadi na hati ya malipo itabandikwa stempu siku ya utekelezaji au tarehe ya hati.
Viwango Vinavyotumika kwa hati mbalimbali
Ushuru wa Stempu unatozwa kwa hati maalum katika viwango tofauti. Baadhi ya hati chache maarufu na viwango vyao vya ushuru ni kama ifuatavyo:
Maelezo ya Hati | Ushuru wa Stempu |
HATI YA KIAPO, Pamoja na uthibitisho au tamko kuhusu watu kwa sheria inayoruhusu kuthibitisha au kutamka badala ya kutoa kiapo. | ShT. 2000/= |
MAKUBALIANO AU HATI YA MKATABA | ShT. 2000/= |
MAKUBALIANO KUHUSU KUWEKA HATI ZA VIWANJA, UBUNIFU, RAHANI AU AHADI | ShT. 2000/= |
UKADIRIAJI AU UTHAMINISHAJI, uliofanyika vinginevyo tofauti na amri ya Mahakama wakati wa shauri: | ShT.500/= |
Hati ya MAUZO YA MALI | Asilimia 0.5 ya ShT. 100,000/= za kwanza, kisha asilimia 1 ya thamani inayozidi ShT. 100,000/= |
MKATABA WA KUPANGISHA, pamoja na mkataba wa kupangisha unaotolewa na mpangaji kwa mpangaji mwingine na mkataba wowote wa kupangisha au kupangishwa na mpangaji wa kwanza: | Asilimia moja ya kodi ya mwaka iliyopokelewa kwa ajili ya pango kwa muda wote |
KATIBA YA KAMPUNI | ShT. 10,000/= |
Hati za UBIA: (i) Iwapo mtaji hauzidi TSH. 10,000/=. (ii) Iwapo mtaji unazidi TSH. 100,000/= lakini hauzidi TSH. 1,000,000/=. (iv) Katika hali nyingine yoyote. Kuvunja ubia. | ShT. 1,000/= ShT. 5,000/= ShT. 10,000/= ShT. 10,000/= |
MADARAKA YA WAKILI, | ShT. 2000/= |
UHAMISHAJI (uwe unazingatia au bila kuzingatia) (a) wa hisa katika kampuni iliyoshirikishwa au shirika lolote; (b) wa karadha iwapo karadha inalipiwa ushuru au hapana; (c) wa riba yoyote iliyopatikkana kutokana na dhamana, mkataba wa dhamana au hati ya bima | Asilimia moja ya thamani ya hisa zilizoidhinishwa na Bodi asilimia moja ya thamani ya hisa zilizoidhinishwa na Bodi asilimia moja ya thamani ya hisa zilizoidhinishwa na Bodi. |
USHURU WA STEMPU
Elewa kuhusu Ushuru wa Stempu
Sheria ya Ushuru wa Stempu, 1972 ilianza kutumika mnamo mwezi Julai 1, 1972. Ilitangua Sheria ya Stempu. Malengo yake yaliwekwa kuunganisha na kurekebisha sheria inayohusiana na ushuru wa stempu, kwa kuweka marekebisho madogo, mengi yao yalikuwa ya kiutaratibu. Masharti yanayohusiana na mikataba ya pamoja yalifafanuliwa. Masharti maalum yanayohusiana na makosa yaliingizwa.
Nyaraka zipi zinahusishwa na Ushuru wa Stempu?
Nyaraka za kisheria zilizofafanuliwa kwenye jedwali ambazo zilizotumika Tanzania bara au kama zilivyotumika nje ya Tanzania bara zinazohusiana na mali yoyote au masuala yoyote au jambo lililofanyika Tanzania bara, lazima zitozwe ushuru kiasi ambacho kimetajwa au kukokotolewa kwa namna ilivyoelezwa kwenye jedwali kuhusiana na sheria hiyo isipokuwa kama zina msamaha wa Ushuru wa Stamp.
Sheria ya Ushuru wa Stempu inabainisha watu watakaolipa ushuru wa stempu ambapo mara nyingi hulipwa na mtu anayeandika, kuandaa au kutumia waraka wa kisheria. Iwapo mtu anakuwa na mashaka kama iwapo waraka wa kisheria unapaswa au haupaswi kubandikwa stempu au kuhusu kiasi cha Ushuru wa Stempu kinacholipwa kuhusiana na waraka wowote wa kisheria, anaweza kupeleka suala hilo kwa Afisa Ushuru wa Stempu kwa ajili ya uamuzi.
Usimamizi wa Ushuru wa Stempu
Wakati ambapo Hati Zinapaswa Kubandikwa Stempu
Hati zote zinazotozwa ushuru wa stempu zinazotumiwa na mtu yeyote Tanzania Bara zinapaswa kubandikwa stempu ndani ya siku thelathini za kutumika:
Iwapo hati imeletwa kwa afisa husika kwa ajili ya uamuzi, inapaswa kubandikwa stempu ndani ya siku thelethini, tangu wakati wa uwasilishaji wa hati hiyo kwa afisa husika hadi wakati taarifa itakapomfikia mtu aliyeiwasilisha kuhusu uamuzi wa afisa husika, siku hizo zitaondolewa katika kukokotoa siku hizo thelathini; na kila risiti, kukiri kuhusu deni, taarifa ya ahadi na hati ya malipo itabandikwa stempu siku ya utekelezaji au tarehe ya hati.
Viwango Vinavyotumika kwa hati mbalimbali
Ushuru wa Stempu unatozwa kwa hati maalum katika viwango tofauti. Baadhi ya hati chache maarufu na viwango vyao vya ushuru ni kama ifuatavyo:
Maelezo ya Hati | Ushuru wa Stempu |
HATI YA KIAPO, Pamoja na uthibitisho au tamko kuhusu watu kwa sheria inayoruhusu kuthibitisha au kutamka badala ya kutoa kiapo. | ShT. 2000/= |
MAKUBALIANO AU HATI YA MKATABA | ShT. 2000/= |
MAKUBALIANO KUHUSU KUWEKA HATI ZA VIWANJA, UBUNIFU, RAHANI AU AHADI | ShT. 2000/= |
UKADIRIAJI AU UTHAMINISHAJI, uliofanyika vinginevyo tofauti na amri ya Mahakama wakati wa shauri: | ShT.500/= |
Hati ya MAUZO YA MALI | Asilimia 0.5 ya ShT. 100,000/= za kwanza, kisha asilimia 1 ya thamani inayozidi ShT. 100,000/= |
MKATABA WA KUPANGISHA, pamoja na mkataba wa kupangisha unaotolewa na mpangaji kwa mpangaji mwingine na mkataba wowote wa kupangisha au kupangishwa na mpangaji wa kwanza: | Asilimia moja ya kodi ya mwaka iliyopokelewa kwa ajili ya pango kwa muda wote |
KATIBA YA KAMPUNI | ShT. 10,000/= |
Hati za UBIA: (i) Iwapo mtaji hauzidi TSH. 10,000/=. (ii) Iwapo mtaji unazidi TSH. 100,000/= lakini hauzidi TSH. 1,000,000/=. (iv) Katika hali nyingine yoyote. Kuvunja ubia. | ShT. 1,000/= ShT. 5,000/= ShT. 10,000/= ShT. 10,000/= |
MADARAKA YA WAKILI, | ShT. 2000/= |
UHAMISHAJI (uwe unazingatia au bila kuzingatia) (a) wa hisa katika kampuni iliyoshirikishwa au shirika lolote; (b) wa karadha iwapo karadha inalipiwa ushuru au hapana; (c) wa riba yoyote iliyopatikkana kutokana na dhamana, mkataba wa dhamana au hati ya bima | Asilimia moja ya thamani ya hisa zilizoidhinishwa na Bodi asilimia moja ya thamani ya hisa zilizoidhinishwa na Bodi asilimia moja ya thamani ya hisa zilizoidhinishwa na Bodi. |
Habari & Matukio
Ufanisi wa Bandari umeongeza mapato ya Serikali
Mwenyekiti wa Bodi aonyesha njia TRA kuvuka malengo