Emblem TRA Logo
Kodi za Mapato yatokanayo na Ajira

Kuelewa dhana ya Kodi  inayotokana na Ajira

Kodi  inayotokana na Ajira inajulikana  kama Lipa kadiri unavyopata. Hii ni kodi ya zuio kwa waajiriwa wanaotozwa kodi. Chini ya mfumo huu, mwajiri anapaswa kisheria kukata kodi ya mapato kutoka katika mshahara au ujira  wa mwajiriwa anayestahili kutozwa kodi.

Maana ya Mwajiriwa:

Mwajiriwa ni mtu anayehusika na ajira inayoendeshwa na mwajiri. Ajira inahusisha waajiriwa wa kudumu, waajiriwa wa muda, meneja, Mkurugenzi, na vibarua. Waajiriwa wanaweza kuajiriwa na mwajiri mmoja au zaidi (ajira ya msingi na ya ziada)

Maana ya mwajiri:

Mwajiri ni mtu anayeendesha, aliyeendesha au ana lengo la kuendesha ajira kwa watu.

Mkurugenzi wa ajira ya kudumu:

Maana yake ni mwajiriwa wa kudumu katika shirika anayefanya kazi ya kiutawala.

Usimamizi wa Kodi ya Mshahara

Mwajiri anapaswa kuzuia kodi ya mapato kutoka katika mishahara, ujira na malipo mengine yote yanayopaswa kukatwa kodi kutoka kwa waajiriwa.

 

Ni Mapato gani yanayohusishwa katika kukokotoa kodi itokanayo na Ajira?

Faida zinazohusishwa katika kukokotoa mapato kutoka katika ajira

 

Mapato ya ajira yanahusisha;

  1. Malipo ya ujira, mshahara, malipo ya likizo, ada, kamisheni, bonasi, kiinua mgongo au posho yoyote ya safari, burudani au malipo mengine yoyote yanayohusiana na ajira au huduma inayotolewa.
  2. Malipo yanayoonesha msamaha au marejesho ya matumizi ya mtu binafsi au mtu mwingine anayehusiana na mtu huyo.
  3. Malipo kwa mkataba wa mtu binafsi katika masharti yoyote ya ajira
  4. Michango na malipo ya kustaafu
  5. Malipo ya kupunguzwa, kupoteza au kufukuzwa kazi
  6. Malipo mengine yanayolipwa yanayohusiana na ajira ikiwa ni pamoja malipo yasiyokuwa ya fedha yanayopatikana kwa mujibu wa sheria
  7. Malipo mengine kama itakavyoonekana yanahitaji kuhusishwa
  8. Malipo ya mwaka anayolipwa mkurugenzi tofauti na malipo yake ya kawaida kama mkurugenzi

Mapato yasiyohusishwa katika kukokotoa kodi inayotokana na ajira

mapato yafuatayo hayatahusishwa katika kukokotoa kodi inayotokana na ajira:

  1. Kiasi kilichosamehewa na malipo ya mwisho ya zuio;
  2. Huduma za kafeteria zinazotolewa bila ubaguzi;
  3. Huduma za afya, malipo ya huduma za afya na malipo ya bima kwa huduma za afya ikizingatiwa kwamba huduma au malipo hayo:
    • Yanapatikana ili kukidhi matibabu ya mhusika, mwenza wake na hadi watoto wao wanne; na
    •  yanawezeshwa kupatikana na mwajiri (na mtu yeyote anayehusiana na mwajiri anayeendesha biashara kama hiyo au inayohusiana na hiyo) katika misingi isiyo ya kiubaguzi;
  4. Posho yoyote ya kujikimu, safari, burudani au posho nyingine zinazohusisha urudishaji wa gharama kwa mnufaika kwa kiwango chochote alichotumia na kisichohusiana na uzalishaji wa kipato chake katika ajira au huduma inayotolewa; 
  5. Faida inayotokana na matumizi ya chombo cha moto ambapo mwajiri hadai kufanya makato yoyote au nafuu kuhusiana na umiliki, matengenezo au uendeshaji wa chombo cha moto;
  6. Faida inayotokana na matumizi ya maeneo ya makazi kwa mwajiriwa wa serikali au taasisi nyingine ambayo bajeti yake haitokani na ruzuku inayotolewa na serikali;
  7. malipo ya safari kwa   mwajiriwa, mwenza wake, na hadi watoto wanne kwenda na kurudi eneo la kazi, yanayoendana na gharama halisi za usafiri ikiwa mwajiriwa anaishi zaidi ya maili 20 kutoka katika kituo chake cha kazi na ameajiriwa kutoa huduma kwa mwajiri katika eneo la kazi;
  8. Mchango na malipo ya kustaafu yanayosamehewa chini ya sheria ya Huduma za jamii za Mafao ya Kustaafu

          9. Malipo yasiyokuwa na sababu za msingi au yasiyotekelezeka                 kiutawala kwa mwajiri kuyajengea hoja au kuelekeza kwa                       wanufaika wao 

          10. Posho inayolipwa kwa mwajiriwa anayetoa huduma binafsi                   ndani ya taasisi kwa wagonjwa katika hospitali za umma; 

         11. Posho ya nyumba, usafiri, uwajibikaji, kazi za ziada, kazi za                   muda wa ziada (ajari), mazingira magumu, na honoraria                       inayolipwa kwa waajiriwa wa serikali au taasisi, bajeti ambayo               inalipwa yote au sehemu yake na ruzuku ya bajeti ya serikali

Mafao ya huduma ya mali


Haya ni mafao yasiyokuwa ya kifedha ambayo mwajiriwa anapewa na mwajiri. Mafao haya yanatathminiwa na sheria na kuhusishwa katika mapato ya kodi ya mwajiri. Yanatathminiwa kwa taratibu zifuatazo:


a)  Utoaji wa nyumba / makazi kwa mwajiriwa:                                                        
Mafao yasiyohusisha fedha yanayohusiana na nyumba/makazi yanachukuliwa kwa kuzingatia kiwango cha chini cha kodi ya nyumba kilichopo na kiwango cha juu katika vipengele vifuatavyo:
15% ya jumla ya kipato cha mwaka  cha mwajiriwa na
Matumizi yatakayodaiwa na mwajiri kama makato yanayohusiana na nyumba


Kumbuka: 
Ikiwa mwajiriwa atachangia sehemu ya kodi inayolipwa kwa ajili ya nyumba, kiwango cha mafao stahiki kitapunguzwa kwa kuzingatia kiasi cha kodi alicholipa mwajiriwa.


b)    Utoaji wa gari kwa mwajiriwa
Ukokotoaji wa Mafao ya mali kutokana na chombo cha moto unazingatia ujazo wa injini na muda ambao chombo kimetumika: Viwango vifuatavyo vitazingatiwa kwa mwaka:
 

Ujazo wa injini

Kuanzia kutengenezwa hadi miaka 5   (ShT)

Zaidi ya miaka 5 (ShT)

Isiyozidi cc 1000

250,000

125,000

Zaidi ya cc1000cc lakini isiyozidi cc 2000

500,000

250,000

Zaidi ya cc 2000cc lakini isiyozidi cc 3000

1,000,000

500,000

Zaidi ya cc3000

1,500,000/=

750,000


Kumbuka:
Mafao ya usafiri hayatahusika ikiwa mwajiri hatadai kufanya makato kwa kuzingatia umiliki, matengenezo, au gharama za uendeshaji wa chombo husika cha moto

c)    Utoaji wa Mkopo kwa Mwajiriwa
Mwajiri anapotoa mkopo kwa mwajiriwa na mkopo huo ukiwa katika kiwango cha riba, chini ya kiwango cha kisheria kiasi cha mafao kwa njia ya mali kinachukuliwa kama tofauti ya haya yafuatayo:
 Kiasi cha riba ambacho kingekuwa kimelipwa endapo riba ya mkopo ingetozwa katika kiwango kilichowekwa kisheria; na
 Kiasi cha riba ya mkopo kilicholipwa kwa mkopo katika kiwango kilichotolewa.
Upekee katika utoaji wa mkopo kwa mwajiriwa
Pale ambapo mwajiri anatoa mkopo ambao kipindi cha kulipwa kwake ni chini ya miezi 12 na jumla ya mkopo wote na malimbikizo ya mikopo mingine kama hiyo ya kipindi chochote ndani ya miezi 12 ya awali hayazidi mshahara wa msingi wa miezi mitatu wa mwajiriwa, basi hakutakuwa na mafao.


d)   Utoaji wa mafao ya huduma nyingine za mali 
Thamani ya soko itatumika katika ukokotoaji wa manufaa  mengine yanayotokana na  mali.
Vikokotoo  vya Kodi ya Ajira  kwa Tanzania Bara na Zanzibar
Viwango vya kodi vinavyotumika kwa Tanzania Bara ni tofauti na vya Tanzania Visiwani. Unakumbushwa kutumia vikokotoo mwafaka vya kodi ya Ajira.
 

Vikokotoo vya Kodi ya Mshahara kwa Tanzania Bara na Zanzibar

Viwango vya kodi ya mapato vinavyotumika kwa mkazi mahususi vinavyotozwa Tanzania Bara ni sawa na vile vinavyotozwa Zanzibar.Unaweza kuangalia kikokoto cha kodi hapa chini:

Vikokotoo  vya Kodi ya Mshahara 

Ajira ya Ziada

Pale mtu anapoajiriwa katika nafasi zaidi ya moja za ajira, basi nafasi za ajira zilizochaguliwa na mwajiriwa huyo na kuchukuliwa kama siyo vyanzo vya msingi vya kipato zinaitwa ajira za ziada.

Waajiri wote wanapaswa kuzuia kodi ya mapato  lakini waajiri wa ziada wanatakiwa kuzuia kwa namna tofauti na mwajiri mkuu.

Wajibu wa Mwajiriwa mwenye Ajira ya Ziada:

(i)Kuchagua, miongoni mwa nafasi za ajira, ipi itakuwa ajira ya msingi na nyingine zitakuwa ajira za ziada

(ii)Kutoa taarifa kwa wakati kwa mwajiri mkuu na waajiri wengine, ambao ni waajiri wa ziada wa mwajiriwa.

Wajibu wa mwajiri:

(i)Kukokotoa kodi kwa kiwango cha juu katika  viwango vya kodi vinavyotumika kwa mtu binafsi.

(ii)Kuwachunguza waajiriwa wote katika kipindi kisichopungua miezi sita, kama wana  ajira ya ziada au la.

Zingatia:

Iwapo kuzuia kodi ya mapato katika kiwango cha juu kutasababisha ugumu wa maisha kwa mwajiriwa, mwajiriwa anaweza kutuma maombi kwa kamishna kuomba amruhusu mwajiri wa ziada atumie kiwango cha chini  katika kuzuia kodi. 

Wafanyakazi wa Ndani ya Nchi wafanyao kazi katika Ofisi za Jumuia ya Madola, Ubalozi na Ujumbe Maalum wa Kidiplomasia

Kwa ujumla ofisi za Jumuiya ya Madola, Kibalozi na Ujumbe Maalum wa Kidiplomasia haziwajibiki kulipa kodi yoyote kwa kuwa zina kinga ya kibalozi na sheria ya Haki za Kidiplomasia. Kwa msingi huo mashirika hayo hayalazimiki kutumia mifumo ya Kodi ya mshahara. Hata hivyo, baadhi ya mashirika yanaamua kutumia mfumo huo ili kutunza nyaraka zao vizuri na kuwasaidia waajiriwa wao kuepuka kupoteza muda wa kushughulikia masuala yao ya kodi na kuzingatia zaidi wajibu wao katika ofisi zao.

Viwango Maalum vya Kodi Vinavyotumika katika Baadhi ya Makundi ya Waajiriwa

Baadhi ya makundi ya waajiriwa yanashughulikiwa kama makundi maalum tofauti na wafanyakazi wengine wa kawaida; hawa ni waajiriwa wanaotoka nje ya nchi na wakurugenzi ambao si sehemu ya wale wa kudumu:-


Waajiriwa ambao si wakazi:
Kwa Waajiriwa wasio wakazi (kwa mfano, waajiriwa wa muda kutoka nje ya nchi) kodi ya inazuiwa kwa kiwango kimoja cha 15% ya mapato ghafi yatokanayo na ajira. Hili ni zuio la mwisho na kiasi kinachozuiwa kinalingana na wajibu wa mwajiriwa wa kulipa kodi ya mapato, kwa mujibu wa ajira yake.


Wakurugenzi  wasio  wa kudumu:
Kodi inazuiwa kwa kiwango cha 15% ya malipo wanayolipwa wakurugenzi wasio wa kudumu. Kiasi cha Kodi inayolipwa ni kodi ya zuio isiyo ya mwisho.
Nyuma

Nyaraka gani zinatakiwa kutunzwa na Mwajiri?

Nyaraka hizo ni pamoja na akaunti, tathmini, kitabu, hati, madai, maelezo, notisi, maagizo, kumbukumbu, taarifa ya kodi au maamuzi na zinaweza kuwa katika muundo wa kielektroniki.

Mwajiri anapaswa kutunza nyaraka zifuatazo:

  • Orodha za walipwa ujira na vocha za mishahara; na
  • Vitabu vingine vyovyote, nyaraka na kumbukumbu zozote zinazohusu ukokotoaji au malipo kwa waajiriwa au kodi iliyozuiwa kutoka katika malipo hayo.

Mwajiri anapaswa kutunza nyaraka hizi kwa kipindi cha miaka 5 kuanzia mwishoni mwa mwaka wa fedha au miaka ya fedha inayohusiana na kumbukumbu hizo isipokuwa kama Kamishna atabainisha vinginevyo kwa maandishi.

Malipo ya Jumla yanafanyikaje?

Malipo ya Jumla kwa waajiriwa yanaweza kutolewa kama bahashishi, malipo ya likizo, fidia, bonasi, kamisheni nk. ambayo yanaweza kuchukua miezi kadhaa au mwaka mzima. Malipo ya jumla tofauti na malipo ya mwisho yanapaswa kuingizwa katika mwaka wa malipo na kutozwa kodi kwa kuzingatia malipo ya mshahara ya mwezi yaliyorekebishwa kwa mwaka. 
Malipo ya jumla ya mwisho ambayo yanahusisha malipo ya kupunguzwa kazini na malipo mengine kwa kupoteza au kuachishwa kazi yatapaswa kutawanywa kwa kipindi cha miaka sita au miaka halisi ya ajira na yatapaswa kutozwa kodi kama mapato ya miaka hiyo.

Michango katika Mifuko ya Wastaafu Iliyoidhinishwa inashughulikiwaje?

Michango inayotolewa na mwajiriwa/mwajiri katika mifuko ya wastaafu iliyoidhinishwa inapunguzwa kutoka kwenye mshahara ghafi wakati wa kukokotoa kodi ya mshahara. Kiasi cha makato haya ni sawa na pungufu ya:

  • Jumla ya michango ya mwajiriwa; au mwajiri ambapo inapojumuishwa katika kukokotoa malipo ya mwezi yaliyofanyika kwenye mfuko wa wastaafu ulioidhinishwa; na
  •  Kiasi cha malipo kisheria kwenye mfuko.