Ndugu mteja,
Ni furaha yangu kupata fursa hii kuwasilisha kwako Mkataba wa Huduma ya Mteja. Huu ni Mkataba ambao unalenga katika kutoa huduma ambayo tumejipanga kukuhudumia kama Mteja wetu. Mkataba huu umeainisha viwango vya huduma, haki na wajibu wako ambavyo kwa pamoja vinatuwezesha kutimiza matarajio yako.
Tunawajibika kukupatia huduma sahihi na rahisi ambayo haina ubaguzi ili kujenga mahusiano yenye kuaminiana na kuheshimiana. Tunakutambua kama mteja mshirika wetu muhimu katika masuala ya usimamizi wa kodi.
Ninasisitiza tena ahadi ya TRA katika kuhakikisha matarajio yako yanatimizwa leo na wakati wote. Tunakuhimiza "TIMIZA WAJIBU TUKUHUDUMIE IPASAVYO" ili kufikia malengo tuliyojiwekea.
KAMISHNA MKUU
Habari & Matukio
Ufanisi wa Bandari umeongeza mapato ya Serikali
Mwenyekiti wa Bodi aonyesha njia TRA kuvuka malengo