Emblem TRA Logo

Mafunzo ya Mifumo kwa Jumuiya za Kodi

22 May, 2024

Featured Image

Kumekuwa na mafunzo ya aina mbalimbali  kwenye lango la mlipakodi  yaliyoundwa ili kuboresha ujuzi wa vitendo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hasa kuhusu usajili, uwasilishaji wa ritani na matumizi bora ya lango la mlipa kodi kidijitali. Mafunzo haya yanatoa muhtasari wa kina wa utendaji kazi mbalimbali unaopatikana kwenye lango la  mlipakodi, ikijumuisha uwasilishaji wa ritani, kufanya malipo na kupata nyaraka muhimu  za kodi. Mafunzo ya vilabu vya kodi yanasisitiza umuhimu wa kutumia lango la  mlipa kodi ili kurahisisha kazi zinazohusiana na kodi, kupunguza hitaji la matumizi ya karatasi na kutembelea ofisi za TRA  mara kwa mara. Kwa kufahamu vyema  vipengele mbali mbali vya lango la mlipa kodi, walipakodi wanaweza kuboresha ufanisi wao kwa kiasi kikubwa, kupunguza makosa na kuongeza ulipaji wa kodi wa hiari. Lengo kuu la mafunzo haya ni kuwawezesha wanafunzi kujifunza kwaa vitendo na kupata maarifa wanayohitaji ambayo itawapelekea  kusimamia majukumu yao ya kodi kwa ufanisi zaidi, na kukuza mazingira ya kodi ya uwazi na uwajibikaji.