Emblem TRA Logo

TRA IRINGA YATOA ELIMU YA KODI KWA KLABU YA KODI SHULE YA SEKONDARI CHANGARAWE

21 November, 2025

Featured Image

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Iringa, mnamo tarehe 20.11.2025, imetoa elimu ya Kodi kwa wanafunzi wa klabu ya Kodi katika shule ya sekondari Changarawe iliyopo  wilayani Mufindi.

Afisa kodi Bw. Shaga Gagunda aliwataka wanafunzi kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za klabu kwa ajili ya kujifunza masuala ya kodi ili wawe mabalozi wema na waaminifu wa hasa katika kudai Risiti kwa manunuzi yote wanayofanya.