WANACHAMA YA VILABU VYA KODI WATOA ELIMU YA KODI MAONESHO YA SABASABA
08 July, 2026
WANACHAMA YA VILABU VYA KODI WATOA ELIMU YA KODI MAONESHO YA SABASABA
Matukio katika Picha ya Wanafunzi wa Vilabu vya Kodi kutoka shule mbalimbali na vyuo vikuu wakishiriki katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya SABASABA, kwa kutoa elimu kuhusu masuala ya kodi kwa wananchi na wanafunzi wanaotembelea maonesho hayo.
Kupitia ushiriki wao, wanafunzi hao wamekuwa wakitoa elimu na ufafanuzi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari, kudai risiti za EFD pamoja na kutambua mchango wa kodi katika maendeleo ya Taifa. Ushiriki huo pia umewapa fursa ya kuongeza uelewa na uzoefu wa vitendo kuhusu masuala ya kodi.
Ushiriki wa Vilabu vya Kodi katika Maonesho ya SABASABA unaendelea kuwa sehemu muhimu ya juhudi za kujenga kizazi chenye uelewa wa masuala ya kodi na kuimarisha utamaduni wa ulipaji kodi kwa hiari, sambamba na kuhamasisha vijana kuwa mabalozi wa elimu ya kodi katika jamii.
Habari Mpya