ELIMU YA DAWATI LA UWEZESHAJI BIASHARA KWA WANAFUNZI WA CHUO CHA EXCELLENT
21 November, 2025
Mkuu wa kitengo cha uwezeshaji biashara Bw. Tumaini Kichila akiongozana na maafisa wengine wa Mkoa Kikodi wa Tegeta, mnamo tarehe 20/11/2025 walikutana na wanafunzi wa chuo cha Exellent kilichopo eneo la Boko ili kuwaelimisha juu ya dawati la uwezeshaji biashara, ulipaji kodi sahihi, huduma zinazotolewa na TRA na kuwaelezea umuhimu wa kujisajili na kuwa na namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN).
Wanachuo hao walipongeza jitihada za mkoa za kuwasogelea mpaka maeneo ya vyuoni, waliomba elimu zaidi ya mambo yahusiyo kodi na kuwekwa kambi chuoni hapo ili waweza kujisajili na kupata TIN