MAKAMU WA RAIS KUWA MGENI RASMI MKUTANO WA 46 WA MAMLAKA ZA KODI JUMUIYA YA MADOLA - DCG
21 September, 2026
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa 46 wa Chama cha Wasimamizi wa Kodi cha Jumuiya ya Madola (CATA), utakaofanyika jijini Arusha na kuwakutanisha viongozi na wataalamu wa usimamizi wa kodi kutoka mataifa 48.
Kwa mujibu wa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Mcha Hassan Mcha amesema mkutano huo utafanyika kuanzia tarehe 05 mpaka 09 mwaka 2026.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Naibu Kamishna Mkuu ameitaja kauli mbiu ya mkutano huo kuwa ni “Matumizi ya Teknolojia katika Kuboresha Ufanisi wa Ukusanyaji wa Mapato,” ambayo inalenga kuhimiza matumizi ya teknolojia katika kuboresha huduma, usimamizi wa walipa kodi na kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato.
Kwa mujibu wa Mcha, mkutano huo unatarajiwa kuleta manufaa makubwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ikiwemo kubadilishana uzoefu na mamlaka nyingine za kodi kuhusu mbinu bora za ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa kodi.
Amesema pia mkutano huo utatoa fursa kwa wataalamu wa TRA kujenga uwezo na kupata maarifa mapya, hususan katika matumizi ya teknolojia, uchambuzi wa taarifa na ubunifu katika usimamizi wa kodi.