TRA ITAENDELEA KUSIKILIZA NA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WALIPAKODI
20 August, 2026
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, amesema Mamlaka itaendelea kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili walipakodi ili kuweka mazingira rafiki ya biashara na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.
Akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Buzuruga jijini Mwanza, Kamishna Mkuu Mwenda amesema TRA inatambua umuhimu wa wafanyabiashara katika kuchangia maendeleo ya Taifa, hivyo Mamlaka itaendelea kuwafikia, kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya kodi.
Amesisitiza kuwa wafanyabiashara wanapaswa kutekeleza wajibu wao wa kikodi kwa usahihi, ikiwemo kutoa na kudai risiti sahihi za EFD, huku akiwataka kutumia fursa za elimu na huduma zinazotolewa na TRA ili kupata uelewa zaidi kuhusu taratibu za kodi.
Aidha, amewahakikishia wafanyabiashara hao kuwa TRA itaendelea kushirikiana nao katika kutatua changamoto zao na kuboresha huduma, akiwataka kutoa taarifa kuhusu changamoto au vikwazo wanavyokutana navyo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kikodi.
Habari Mpya