KAMISHNA MKUU WA TRA ASHIRIKI MKUTANO WA 18 WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI WA EAC ARUSHA
15 May, 2026
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, ameshiriki Mkutano wa 18 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (East African Community (EAC)) unaofanyika jijini Arusha, ukiwakutanisha viongozi na wataalamu kutoka nchi wanachama kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi na kifedha katika ukanda wa Afrika Mashariki. Mkutano huo umejikita katika kuimarisha sera za fedha, usimamizi wa uchumi pamoja na kuendeleza ajenda ya ujumuishaji wa kifedha kwa manufaa ya wananchi wa Jumuiya hiyo.
Katika majadiliano hayo, wajumbe wameangazia mikakati ya kukuza biashara na uwekezaji kati ya nchi wanachama, kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato pamoja na kuongeza ufanisi wa taasisi za kifedha. Vilevile, wamejadili namna bora ya kuboresha mazingira ya biashara ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kuongeza ushindani wa kikanda.
Mkutano huo pia umesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu wa kikanda katika kukabiliana na changamoto za kiuchumi zinazoikabili Afrika Mashariki, sambamba na kuimarisha mifumo endelevu ya ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi wa nchi wanachama.
Habari Mpya