RAIS MWINYI AMEKUWA NGUZO MUHIMU KATIKA UKUSANYAJI WA MAPATO - CG MWENDA
18 March, 2026
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hussein Ali Mwinyi, kwa kuwa mstari wa mbele katika kuiwezesha TRA kutekeleza majukumu yake.
Shukrani hizo ziliambatana na kukabidhi zawadi maalum ya kutambua mchango huo, ambayo ilipokelewa kwa niaba ya Rais Mwinyi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdullah, wakati wa hafla ya Iftari iliyoandaliwa na TRA tarehe 17 Machi 2026, Visiwani Zanzibar.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Abdullah ameeleza kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na TRA katika ukusanyaji wa kodi, na itaendelea kuiunga mkono ili iweze kutekeleza wajibu wake muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Aidha, alisisitiza kuwa kila mwananchi anao wajibu wa kulipa kodi, akibainisha kuwa vitendo vya ukwepaji kodi havitavumiliwa na wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Habari Mpya