MAENDELEO YALIYOTUZUNGUKA TZ NI MATOKEO YA KODI - MAKAMU WA PILI WA RAIS SMZ
18 March, 2026
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah amesema maendeleo yanayoonekana katika kila kona ya nchi yanatokana na makusanyo ya Kodi hivyo kila mwananchi anapaswa kuchangia maendeleo hayo kwa kulipa kodi.
Ameyasema hayo leo Machi 17.2026 wakati wa Iftari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Zanzibar nakuwakutanisha watumishi wa TRA na Walipakodi katika hoteli ya Madinat Al Bahr Zanzibar.
Amewapongeza TRA kwa kuendelea kukusanya kodi kwa weledi na kuvuka malengo inayowekewa na Serikali.
"Hatuwezi kuacha kusema kazi nzuri inayofanywa na TRA ikiongozwa na Kamishna wake mkuu ambaye amekuwa mstari wa mbele kuweka mazingira mazuri ya ulipaji kodi kwa kuzungumza na Walipakodi" amesema Makamu wa Pili wa Rais SMZ.
Aidha amewataka walipakodi kufuata sheria za kodi zilizowekwa na Serikali ili kuchangia maendeleo ya Taifa ambayo yanamnufaisha kila mwananchi.