Emblem TRA Logo

CG MWENDA AKUTANA NA UONGOZI WA TWIGA CEMENT KUJADILI SUALA LA BEI YA SARUJI

17 September, 2026

Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Yusuph Juma Mwenda, amekutana na uongozi wa Twiga Cement jijini Dar es Salaam kujadili suala la bei ya saruji nchini. Amesema TRA ina jukumu la kuwezesha biashara na itaendelea kushirikiana na wazalishaji katika kutatua changamoto za kikodi.

Amesema TRA itaendelea kufuatilia mnyororo wa uzalishaji na uuzaji wa saruji nchini ili kubaini changamoto zinazoweza kuathiri biashara. Pia amejionea mwenendo wa uzalishaji kiwandani hapo.

Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi wa Twiga na Simba Cement, Mhandisi Danford Semwenda, amesema viwanda vyao havijapandisha bei ya saruji na uzalishaji unaendelea kama kawaida. Amesema kampuni imefuatilia mwenendo wa bei sokoni na kubaini kuwa bei katika viwanda vyao haijabadilika.

Mhandisi Semwenda amesema kampuni inaendelea kuzalisha na kusambaza saruji kwa bei iliyopo, huku ikiendelea kufuatilia mwenendo wa soko. Twiga Cement na Tanga Cement ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa saruji nchini