Emblem TRA Logo

RAIS WA CATA AIPONGEZA TANZANIA NA TRA KWA MAANDALIZI NA USIMAMIZI MZURI WA MKUTANO WA 46

08 October, 2026

Rais wa Chama cha Mamlaka za Mapato za Jumuiya ya Madola (CATA), Dkt. Abu Tariq Jamaluddin, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha kufanyika kwa Mkutano wa 46 wa CATA nchini Tanzania, lakini kuwapongeza Mamlaka ya mapato Tanzania kuandaa mkutano huu muhimu uliozikutanisha mamlaka za mapato kutoka nchi mbalimbali kujadili matumizi ya teknolojia katika kuboresha ukusanyaji wa mapato na huduma kwa walipakodi.

Dkt. Jamaluddin amesema Tanzania imeonesha dhamira ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika usimamizi wa mapato, huku mkutano huo ukiwa fursa ya kubadilishana uzoefu, maarifa na mbinu bunifu za kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani.

Amesisitiza kuwa matumizi ya teknolojia ni kiungo muhimu cha kuleta chachu ya makusanyo ya kodi na kurahisisha huduma za kodi huku akitoakutoa hamasa kwa nchi zote washiriki kuendelea kuona namna ya kuboresha mifumo ya teknlolojia kwenye shughuli za ukusanyaji wa mapato.

Aidha, ametoa pole kwa Mhe. Rais Samia na Watanzania kufuatia msiba uliotokea, akieleza masikitiko yake na kuwapa pole wote walioathirika na msiba huo.

Amehitimisha kwa kusisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano na mshikamano miongoni mwa nchi wanachama wa CATA ili kukabiliana na changamoto za usimamizi wa mapato na kujenga mifumo ya kodi yenye ufanisi, haki na tija kwa maendeleo ya nchi.