Emblem TRA Logo

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inawezesha upatikanaji wa tovuti hii pamoja na taarifa, maudhui, nyenzo na huduma zote zilizomo ndani yake “kama ilivyo” na “kama inavyopatikana”, bila dhamana za aina yoyote, iwe ni za moja kwa moja, za kudokeza au za kisheria, ikiwa ni pamoja na (lakini si tu) dhamana ya usahihi, ukamilifu, kutegemeka, wakati muafaka, kutokukiuka haki, uuzaji au kufaa kwa madhumuni maalum.

 

Kwa kiwango cha juu kinachoruhusiwa na sheria zinazohusika, TRA inakanusha waziwazi dhima yoyote ikiwemo hasara yoyote ya moja kwa moja, isiyo ya moja kwa moja, ya kawaida, ya matokeo, maalum au ya mfano, ikiwa ni pamoja na (lakini si tu) upotevu wa data, upotevu wa mapato, upotevu wa faida, au kukatizwa kwa biashara, inayotokana na au kuhusiana na matumizi, kutoweza kutumia, au kutegemea taarifa au nyenzo zozote zilizo kwenye tovuti hii.

 

TRA haitoi dhamana kwamba tovuti hii itapatikana wakati wote bila kukatizwa, kwa usalama, bila makosa, au bila ya kuingiliwa na virusi / programu hasidi au vipengele vingine vyenye madhara, au kwamba dosari zote zitarekebishwa.

 

Tovuti hii inaweza kuwa na viungo vinavyoelekeza kwenye tovuti au nyenzo za wahusika wengine. Viungo hivyo vimewekwa kwa ajili ya urahisi wa upatikanaji na madhumuni ya kutoa taarifa tu. TRA haina udhibiti wala haiwajibiki kwa maudhui, usahihi, uhalali, upatikanaji au uendeshwaji wa tovuti zozote za wahusika wengine. Kujumuishwa kwa viungo hivyo hakumaanishi uidhinishaji, ufadhili au idhini kutoka kwa TRA. Watumiaji wanafungua au kutumia tovuti hizo za nje kwa hatari yao wenyewe.

 

Ingawa TRA inajitahidi kuhakikisha kuwa taarifa zote zinazochapishwa kwenye tovuti hii ni sahihi na zinasasishwa, TRA haita wajibika kwa makosa yoyote, upungufu au kutokuwa sahihi. Watumiaji wanashauriwa kuthibitisha taarifa wenyewe kabla ya kuzitegemea katika matumizi.

 

Hakuna kilichomo katika kanusho hili kitaweza kuzuia wala kupunguza dhima yoyote ambayo haiwezi kuzimwa au kupunguzwa chini ya sheria zinazotumika za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.